RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

24.12.2017: NAIBU WAZIRI KILIMO MHE. DKT. MARY MWANJELWA ATOA SALAMU ZA KRISMASI KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Haya ndiyo aliyoyasema Naibu Waziri Kilimo, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (MP) katika ibada ya maandalizi ya mkesha wa Krismasi iliyofanyika Katina kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” siku ya Jumapili 24.12.2017. Alianza kwa kusema hivi, Bwana Yesu asifiwe sana kanisa. ninawapenda. Ninamshukuru sana mbeba maono wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa namna anavyoliendesha kanisa hili. Pia huwa nabarikiwa sana na kipindi cha Saa ya faraja ambacho hurushwa na televisheni ya Channel 10 kila alhamisi. Hakika kama kanisa huwa mnanibariki sana na kuinua imani yangu. Na tena niwapongeze kwaajili ya kongamano la SHILO 2017 ambalo limekuwa ni baraka hapa kanisani na kila kona ya dunia hii. Na mimi nimemuona BWANA kupitia kongamano la SHILO, hakika kanisa linafanya kazi nzuri sana kwa utukufu wa MUNGU.

Na pia huwa nabarikiwa sana kuona jinsi mnavyomuombea mpendwa wetu Rais na Nabii Dkt. John Pombe Magufuli. Hakika Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare Mungu akubariki sana kwa kumuombea jemedali wetu kwasababu yeye alisimama kama alivyosimama sasa na ndio maana mnaona nchi yetu inasonga mbele na inabarikiwa sana.

Mwisho, natoa salamu zangu za Krismasi kwenu na kwa Watanzania wote, kwasababu Krismasi ni siku ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo, basi nasi tuzaliwe na Yesu Kristo ndani ya mioyo yetu kwa matendo. Mungu wa mbinguni awabariki, tusherekee vyema na kazi zote zinazofanyika mahali hapa zizidi kubarikiwa kwasababu kupitia kazi hizi tunamuona BWANA na watu wanafunguliwa na vifungo vya shetani. Asanteni”
Naibu Waziri Kilimo, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (MP)
















Comments