Ilikuwa siku ya maandalizi ya mkesha wa KRISMASI Jumapili 24.12.2017 ambapo wamama wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" walipoweza kutoa zawadi ya KRISMASI kwa wachungaji zaidi ya 10 wa kanisa hilo kama shukrani kwa mafundisho mema walioyatoa kwa takribani mwaka mzima. Wamama hawa ambao wanasifika kwa moyo wao wa upendo, walimshukuru sana mbeba maono Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa kuwaambukiza ule moyo wa kuwapenda watu bila kujali dini, kabila, rangi au hali yao ya kiuchumi.
Wamama hawa wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" ambao wanaamini kuwa "Mwanamke ni Jeshi Kubwa" wamekuwa wakishangazwa sana Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa kitendo chake cha kuacha kitanda kwa kipindi fulani na kulala chini akiwaombea waumini na Watanzania wote mafanikio ya kimwili na kiroho. Kitendo hicho kimewajenga sana kiimani na kimewasaidia wamama hawa kuwa na bidii ya kufanya kazi ya Mungu na pia kujibidiisha katika kazi zao za kila siku.
Mzee wa kanisa Rogathe Buhatwa aliwaomba wamama wote kuwa na umoja na ushirikiano katika kufanya kazi ya Mungu. Aliwataka kuondoa matengano na kuachiana kazi bali watu wote wafanye kazi kwa umoja ili kufanikisha kazi ya Mungu.

Mzee wa kanisa Rogathe Buhatwa akiwapongeza wachungaji wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B"
Comments