Mshukuruni BWANA na kila jambo, hata pale unapopitia magumu na majribu makali wewe mshukuru Mungu. Hata unapokuwa katika maisha ya raha, wewe mshukuru Mungu. Kila jambo unalopitia katika maisha yako, Mungu ana mapango nalo, kwahiyo usijutie hiyo hali unayopitia kwani ipo siku utafurahi na kumshangilia huyu Mungu kwa yale utakayotendewa ukiwa bado unaishi hapa duniani. Na wewe ambaye umebarikiwa na vingi usijisahau kumshukuru Mungu, kwani Mungu wetu anakusudi na hayo mafanikio uliyonayo. Kile unachokipa, usisahau kusema, “Asante Mungu”
Siku ya Jumapili 21.01.2018 mama huyu alimshukuru Mungu kwa yale yaliyomkuta katika familia yake. Pia alimshukuru sana Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa jinsi alivyokuwa karibu katika mapito yake na jinsi alivyoweza kumtia moyo na kumfariji. Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" lilibeba jaribu na huyu mama kama mzigo wake mpaka dakika ya mwisho. Vijana na wazee wa kanisa walikuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanakuwa pamoja na huyu mama kwa kumsaidia kimwili na kiroho na kumtia moyo.
Yawezekana umekuwa ukipitia mapito magumu na uko peke yako. Kila ukiangalia kulia na kushoto huoni wa kukusaidia. Inafika kipindi unachanganyikiwa na kuanza kuwaza mawazo mabaya. Nikualike katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" ambalo limekuwa mstari wa mbele wa kusaidiana na kutiana moyo wakati wa mateso na raha. Ibada zetu za Jumapili zinaaanza saa 3 asubuhi hadi hadi saa 8 mchana.
Kanisa limeandaa usafiri wa bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola jijini dar es Salaam, Tanzania. Karibuni sana
//UNAWEZA KU-SHARE POST YETU ILI NA WENGINE WABARIKIWEKAMA WEWE ULIVYOBARIKIWA.//
Comments