RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

18. 02. 2018: MTUMISHI WA MUNGU MARTHA KOMANYA ALIVYOONGOZA KIPINDI CHA SIFA KATIKA IBADA YA KUMILIKI SIKU YA JUMAPILI


//ZABURI 98:1: Mwimbie BWANA wimbo mpya, kwa maana ametenda mambo ya ajabu..//

Hivi ndivyo watu walivyomwimbia Mungu kwasababu ya yale matendo aliyoyafanya katika maisha yao. Hii ilifanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 18.02.2018, waumini na wageni waliofika katika ibada ya KUMILIKI waliweza kumwimbia Mungu wakiongozwa na mtumishi wa Mungu Martha Komnya ngu kwenye kipindi cha sifa. Ilikuwa ni ibada iliyojaa nguvu na uwepo wa Mungu. 

Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa matendo makuu aliyoyafanya kwa watu wake katika kipindi cha sifa. Watu waliweza kujiachia kwa Mungu huku wakiiimba na kucheza mbele za Mungu wakiongozwa na Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare. Hakika ilikuwa ni ibada ya tofauti sana.

Pia tunamshukuru sana Mungu kwa kuona watu wanatambua umuhimu wa kumsifu Mungu kwa Roho na Kweli. Unajua Mungu wetu anapenda sana kuona watoto wake wakimsifu na kumtukuza kila kuitwapo leo. Mungu wetu ni Mungu wa sifa kwahiyo ni wajibu wetu wa kumsifu kila wakati kwa yale matendo mema anayofanya katika maisha yetu. Mungu wetu ametupa pumzi bure, anatulisha, anatupa njia ya kupata fedha, anatufungulia milango ya baraka, anatuepusha na mabaya mengi, anawazomesha watoto wetu, analilinda taifa letu na mambo mengine kama hayo. Hakika Mungu wetu ni waupendo na anastahili kusifiwa na kuinuliwa daima.

Kwahiyo ibada ya sifa isiwe tu kanisani au kwenye mikusanyiko ya watu au kwenye makongamano na semina mbalimbali, bali ifanyike ndani ya mioyo yetu kila wakati na kila mahali. Ni vyema kujipangia muda wako kwaajili ya kumsifu Mungu bila ya kulazimishwa na mtu.

Unapoamua kumsifu Mungu unatakiwa kufanya kutoka ndani ya moyo wako na sio kwa kuwaiga wengine wanapomsifu Mungu. Unatakiwa kumsifu kwa kumaanisha bila kulazimishwa na mtu kuimba au kupiga makofi. 

Mungu atusaidie kutambua umuhimu wa kusifu. Nikukaribishe katika ibada ya Jumapili hii katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Ibada yetu itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. 

Kanisa limekuandalia usafiri wa bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho jijini D'Salaam na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola.

Martha Komanya







 Kulia: Naibu Waziri wa Kilimo Dr. Mary Mwanjelwa


































Comments