RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

18.02.2018: BAADHI YA WATU WALIOKOKA KATIKA IBADA YA KUMILIKI | MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"


Baadhi ya mamia ya watu waliokoka katika ibada ya KUMILIKI iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku Jumapili 18.02.2018. Mch. Francis Machichi aliwaongoza na kuwaombea sala ya toba. Baada ya kuombewa sala ya toba, Mch. Manumbu akishirikiana na wachungaji wengine waliwaombea wangofu wapya na kukema majini na mapepo yaliyokuwa yakiwasumbua kwa mufda mrefu. Baada ya kuombewa walibatizwa kwa maji waliweza kupata vinywaji kanisani hapo na siku ya Jumatatu na Jumanne walianza masomo yao ya kukulia wokovu katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B"

Tunakualika wewe ambaye hujaokoka katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili hii, utaongozwe sala ya toba na kubatizwa kwa maji mengi. Katika Ibada Kuu Mhe.Bishop Dr. Gertrude Rwakatare atakufundisha Neno ambalo litakusaidia kusimama katika wokovu wako, kumjua Mungu kiundani, na kupokea nguvu mpya ittakayokufanya usimame IMARA katika imani yako na wokovu wako.

Amua sasa maana hujui lililo mbele yako. Unatakiwa kutambua kuwa shetani anakuwinda kila siku, kila saa ili akuangamize. hatamani kukuona unafanikiwa maishani mwako bali anatamani kukuona unateseka kila siku.

Kimbilia kwa Yesu Jumapili hii ili uwe katika mikono ya Mungu iliyo salama. Ukiwa na Mungu unapata faraja ya moyo, unabarikiwa, kimwili na kiroho, milango yako ya mafanikio inafunguliwa, unainuliwa katika kazi yako, biashara yako, ofisi yako n.k.
18..02.2018: MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B": WALIOKOKA

Pengine hayo maisha unayoishi si ya kiwango chako. Labda leo hii ungekuwa katika maisha ya furaha, amani, maisha yenye kumtukuza Mungu, lakini hayo yote hajatokea kwako, umekuwa ni mtu wa kuteseka na magonjwa, ulevi, uzinzi, usengenyaji, uongo, utapeli, majivuno, hasira, kutojali jamaa na ndugu zako, magonjwa yamekuandama, unadaiwa, hupati kibali wala promosheni kazini kwako, unafeli masono, huoi wala kuolewa, kauli yako mbaya, mtu wa hasira na mengine kama hayo. Shetani anafurahi sana maisha unayoshi ya mateso wakati Mungu hapendezewi kabisa, anatamani kuona unaisha maisha ya fura kila wakati.

Sasa, Jumapili hii ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Kanisa limeaandaa usafiri wa bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa. karibu sana mtu wa Mungu
 Mch. Francis Machichi akiwaongoza waongofu wapya sala ya toba



Mch. Francis Machichi


































































Comments