RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

25.02.2018. MATUKIO KATIKA PICHA YA WATU WAKIOMBEWA NA KUTOKWA NA MAPEPO KATIKA IBADA YA ISHARA, MIUJIZA NA MAOMBI YA MPENYO

Matukio katika picha ya Ibada ya MIUJIZA, ISHARA NA MAOMBI YA MPENYO iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare siku ya Jumapili 25.02.2018.

Watu waliombewa na wengi wao walitokwa na mapepo, majini, vinyamkera na nguvu za giza zilizokuwa zikiwasumbua kwa muda mrefu. Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aliweza kufanya maombi maalum, kukemea mapepo na nguvu za giza zillizokuwa zikiwatesa watu kwa muda mrefu. Pia aliweza kuwagusa kwa mkono wake baadhi ya maelfu ya watu waliokuwa wamedondoshwa na mapepo wakipiga kelele na kugalagala chini wakihitaji msaada kutoka kwa Mungu baba. Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aliweza kutamka maneno ya AMRI na mapepo na majini yaliweza kutii kwasababu ilikuwa ni AMRI kutoka kwa Mungu wa mbinguni .

Mch.Noah Lukumay ambaye alikuwa kwenye maombi ya kufunga kwa siku 40 aliweza kushambulia mapepo na nguvu za giza kwa kukemea na kutumia jina la Yesu kuharibu kazi za shetani zilizokuwa zikiwasumbua watu kwa kwa muda mrefu. Tulisikia sauti za mapepo zikisema zinataka kutoka katika miili ya watoto wa Mungu kutokana na moto uliokuwa ukiyaunguza wakati wa maombezi.

Tunamshukuru sana Mungu maana watu wengi walishuhudia jinsi Mungu alivyofanya kazi katika miili yao.

Yawezekana unasumbuliwa na nguvu za giza, mapepo na majini. Umekuwa ni mtu wa kulia na kuwa na usongo wa mawazo kutokana na changamoto unazopitia. Yawezekana una mali nyingi lakini umekuwa ni mtu wa majuto na mahangiko, yawezekana ni masikini lakini bado unazidi kutesea. Furaha na amani vimetoweka katika maisha yako umebaki na maumivu na uchungu katika maisha yako. wale uliokuwa unawategemea watakusaidia wamekukimbia, umebaki peke yako. Imefika kipindi unahisi kuvchanganyikiwa na kujiua kutokana na mateso ya dunia hii. Umehangaika bila kupata msaada na matokeo yake umepoteza pesa zako na mali zako kwa kuwalipa waganga wa kienyeji na bado ndoa yako, kazi yako, biashara yako, familia yako, mali zako, malengo yako, uzao wako, masomo yako n.k vyote viko mashakani na umekuwa ni mtu wa kuteseka na kuhangika.

Nataka nikuambie kuwa lipo tumani mbele yako, yako majibu ya maswali yako mbele yako, upo ukombozi mbele yako, kupo kufunguliwa mbele yako. Mtazame Yesu Kristo na kushiriki ibada kila kuitwapo leo. amini kile unachofundishwa na watumishi wa Mungu na kifanyie kazi katika maisha yako. Ondoa hofu ndani ya moyo wako bali jiamini kwasababu umekubali kuwa na Yesu Kristo.

Sasa nikualike katika ibada ya Jumapili hii Mlima wa Moto Mikocheni "B". Ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. kanisa limeandaa usafiri wa bure wa kufika kanisani kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola. Wajulishe na wenzako kwa KU-SHARE ujumbe huu

Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akiombewa watu wenye mapepo na nguvu za giza

















































































David Robert














Comments