RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

11.03.2018: MAOMBI YA KUVUNJA ROHO YA UTSA NA KUTOONGEZEKA YALIVYOFANYIKA KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

TAFAKARI:
//MITHALI 27:1 Usijisifu kwaajili ya kesho; Kwa maana hujui yatakayozaliwa na siku moja.//

Tuna kila sababau ya kumshukuru Mungu kwa wema wake na upendo wake kwetu. Mungu amekuwa mwema katika familia zetu, ndoa zetu, kazi zetu, masomo yetu n.k. Hakika hatustahili kujisifu kwa kuiona siku ya leo maana ni kwa huruma na neema za BWANA tumeweza kuiona siku hii. Kama Wakristo tunapaswa kumuomba sana Mungu kwaajili ya kesho yetu kwa maana kesho yetu ni giza, hatujui litakalozuka kuanzia sasa. Mungu ndiye anayejua kesho yako.

Siku ya Jumapili 11.03.2018 watu wa Mungu walimshukuru Mungu kwa wema wake katika ibada ya KUVUNJA ROHO ZA UTASA NA KUTOONGEZEKA iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na jopo la wachungaji wa kanisa hilo waliongoza maombi ya KUVUNJA ROHO ZA UTASA NA KUTOONGEZEKA. Tunamshukuru Mungu tuliona nguvu za Mungu katika kipindi cha maombi.

Tukukaribishe katika ibada ya Jumapili hii ili ukutane na nguvu za Mungu. Ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Kanisa limeandaa usafiri wa bure wa kufika kanisani kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola

Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare














Mch. Francis Machichi














































Mch. Prisca Charles



























Mch. Stanle Nnko




Comments