RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

23.03.2018: MAONI YA WATU KUHUSIANA NA IBADA YA MAOMBI YA KUKOMESHA ROHO YA MAPOOZA

Baadhi ya watu waliopata nafasi ya kuongea na Mlima wa Moto Online TV na kutoa maoni yao kuhusiana na ibada ya Maombi ya Kukomesha Roho za Mapooza iliyoongozwa na Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare siku ya Jumapili 23.03.2018 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" jijini Dar es Salaam. Watu wengi waliguswa na ibada hii maombi ambayo ilikuwa ni ya tofauti sana ukilinganisha na ibada zilizopita katika kanisa hili. Mungu alitushangaza kwa kulijza kanisa lake na vile alivyokuwa akiwashughulikie kila mtu kulingana na ombi lake. Tunamshukuru sana Mungu kwa kile anachokifanya kwa watu wake na ndio maana hawakubali kukosa kushirikii ibada za Mlima wa Moto Mikocheni "B".

Mlima wa Moto Online TV inaamizi Jumapili hii itaongea na wewe kuhusiana na ibada ya Jumapili hii ambayo itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Tunaamini hutakosa cha kuongea kwasababu katika ibada za kanisa hili kuna ishara na miujiza inayotokea kila siku na watu wanafunguliwa na nguvu za giza. Pia utapata kuelezea kile ambacho umekipata baada ya kusikia ujumbe wa Mungu kupitia mtumishi wake Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare. 

Kanisa limekuandalia usafiri wa bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola. Tunakuomba sana uje na mwanao, mtoto wa jirani yako au ndugu yako, dada wa nyumbani mwako, rafiki yako, ndugu yako ili nao waweze kukutana na baraka za Mungu Jumapili hii. Kwa kufanya hivyo BWANA atakubariki na kukuinua KIROHO na KIMWILI. Ubarikiwe sana.
















Comments