TUTAFAKARI NA TUFANYIE KAZI:
// WAKORITHO 1:9-10 -Mungu ni mwaminifu ambaye mliitwa na yeye mwingie katika ushirika wa Mwanae, Yesu Kristo BWANA wetu. Basi ndugu nawasihi, kwa jina la BWANA wetu Yesu Kristo, kwamba nyote mnene pamoja, wala pasiwe kwenu faraka, bali mhitimu katika nia moja na shauri moja.//
Tukiwa katika maandalizi ya somo zuri la Mch. Sylvanus Komba wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" alilofundisha siku ya Jumapili 23.03.2018 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare tumeona ni vyema ukatafari ujumbe huo hapo juu na kuufanyia kazi katika maisha yako.
Mch. Sylvanus Komba katika mafundisho yake alikemea sana roho mbaya ya uasi makanisani. Kwahiyo tunaamini somo hili litakubariki sana na utakuwa mtu wa tofauti sana. Unajua uasi umetawala sana makanisani, watu wameuzoea wokovu na kuona ni kitu cha kawaida, hawana ile hofu ya Mungu, wanafanya mambo mabaya bila kumuogopa Mungu.Tunatakiwa kuikemea kama Wakristo tunayetamani kwenda mbinguni.
Kwahiyo endelea kufuatilia post zetu ili ujifunze somo zuri kutoka kwa Mch. Sylvanus Komba alilohubiri katika ibada ya maombi ya KUKOMESHA ROHO ZA MAPOOZA.
Mch. Sylvanus Komba kutoka kanisa la Mlima wa Moto Dodoma
Comments