RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

23.03.2018: MHE. BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE AKIOMBEWA KATIKA IBADA YA KUKOMESHA ROHO ZA MAPOOZA

TUTAFAKARI NA TUFANYIE KAZI:

// ZABURI 107:13 - Wakamlilia BWANA katika dhiki zao, akawaponya na shida zao. Aliwatoa katika giza na uvuli wa mauti, akayavunja mafungo yao. //

Kumbe ukimlilia BWANA katika changamoto zako za kimaisha au dhiki zako, BWANA anaziondoa na kuponya shida zako. Kwahiyo upo umuhimu wa kumlili BWANA ili atimize ndoto zetu na haja ya mioyo yetu. Tunapaswa kuwa karibu na Mungu na kuyatenda yale anayopenda tuyatende ili aweze kutusikia katika kilio chetu na kutufuta machozi. Haijalishi wewe una mali nyingi sana au ni maskini sana, kwa Mungu unahitaji kujishusha kwani yeye ndiye aliyetuumba na sisi sote ni sawa mbele za Mungu. Kwahiyo usijione umefanikiwa sana ukasahahu kuomba au ukajiona ni maskini sana ukajidharau na kuacha kuomb. Katika maisha yako tamani sana kuishi maisha ya kumpendeza Mungu na kuyafanya yale yote anayokuagiza katika kitabu chake kitakafu yaani Biblia. Tabia yako njema itakufanya umpendeze Mungu na Yeye atakuwa karibu wakati wa shida zako. Mbele za Mungu jiamini, jithamni na jionyeshe wewe ni wa maana mbele za Mungu bila kuangalia hali yako ya kiuchumi au kiafya.

Jumapili 23.03.2018 waumini wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" waliweza kumuombea Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare pamoja na watoto wake na wajukuu zake katika ibada ya KUKOMESHA ROHO ZA MAPOOZA. Hivi ndivyo inavyotakiwa kwa watu waliokoka kufanya maombi kila wakati ili Mungu aingilie kati katika familia zetu, ndoa zetu, masomo yetu, mashamba yetu, mifugo yetu, afya zetu, mahusiano yetu, uzao wetu n.k. Maombi yetu yanatakiwa kuwa ni maombi ya kumanisha na sio kuiga mkumbo wa watu. Muombe Mungu kwa Roho wa kweli na sio kufanya maombi ya mazoea. Mtangulize Roho Mtakatifu akuongoze katika maombi yako. Unaweza kuomba sana lakini kama huna IMANI na hicho unachokiomba, maombi yako yatakuwa ni bure. Kwahiyo unapoomba maanisha, uwe na imani, tamani Roho Mtakatifu akuongoze kwa yale utakayokuwa unayatamka mbele za Mungu.






















































Comments