RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

23.03.2018: VIONGOZI WA KANISA WAONGEA NA WAUMINI SIKU YA JUMAPILI NA KUWASHUKURU

Katika ibada ya MAOMBI YA KUKOMESHA ROHO ZA MAPOOZA iliyoongozwa na Mhe. Bishop Dr..Gertrude Rwakatare siku ya Jumapili 23.03.2018 ndani ya kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B", viongozi wa wababa, wamama, vijana wa kanisa hilo waliweza kuongea na waumini na kuwahimiza kujiunge katika idara hizo kwani kuna faida nyingi wanaweza kuzipata ikiwa ni pamoja na kujuana na kusaidiana wakati wa shida na raha. Watu wengi wamenufaika baada ya kujiunga na idara hizo na sasa wanafurahia ukuu wa Mungu.

Wewe ambaye hukupata nafasi ya kusikia kile walichokiongea viongozi hawa, tunakualika katika ibada ya Jumapili hii Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana ili uweze kujifunza Neno la Mungu la Jumapili, na baada ya hapo utaweza kuonana na viongozi hawa ili wakuelekeze ni jinsi gani ya kuweza kujiunga na watakupa faida gani utazipata baada ya kujiunga. Pia na wewe ambaye unaabudu katika kanisa hili na bado hujajiunga, unayo nafasi sasa ya kujiunga ili kanisa liweze kukutambua kwa haraka, hata kama kanisa linawatambua watu wote wanaoshiriki ibada za Mlima wa Moto Mikocheni "B" lakini ni vyema ukajiunga na makundi hayo mapema.

VIONGOZI WA WAMAMA WA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"




















VIONGOZI WA WABABA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"






VIONGOZI WA VIJANA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"
































Comments