RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

28.03.2018: MCH. ANTHONY MWAKIBETE KATIKA IBADA YA IJUMAA KUU YA KUSHIRIKI MEZA YA BWANA

Baada ya kushiriki MEZA YA BWANA kwa Kunywa Damu ya Yesu na kula Mkate siku ya Ijumaa Kuu 28.03.2018 ndani ya kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B", sasa tunakukaribisha katika ibada ya JUMAPILI YA PASAKA (EASTER SUNDAY) siku ya Jumapili hii katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare anaomba uje na ZAWADI ambayo ni wewe kuja na mtu mmoja au zaidi katika ibada ya kesho. Hii ni ibada ambayo hufanyika mara moja tu kwa mwaka. Ni siku ya KUFUFUKA kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Ibada hii itakuwa ni ibada ya Jumapili ya Pasaka ya UFUFUO wa vitu vilivyokufa katika maisha yako. 

Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare atakufundisha Neno la Mungu, atakuombea, atakutamkia baraka, kwa wale wanaokoka atawaongoza sala ya toba na kuwababtiza, atagawa mafuta ya upako na kuwagawia waumini wote. Pia kutakuwa na waimbaji kama vile Happy Kway, Joybringers Kwaya, Aniset Butati na Kasaki Seleman.

Kanisa limeandaa usafiri wa bure wa kufika kanisani katika vituo vifuatavyo: Kituo Cha Mabasi Cha Makumbusho, Mwenge Kwenye Mataa Barabara ya Coca Cola,
Ilala stendi, Tegeta Wazo, Goba Stand, Mbezi Mwisho/Kimara Stop Over,
Buguruni Chama/Mandela Road, Mbagala Rangi 3

..........................
// Mch. Antony Mwakibete
// Mlima wa Moto Mikocheni "B"
// Picha za ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Ijumaa.
//Tunawakaribisha wote siku ya Jumapili hii.


Mch. Anthon Mwakibete

Comments