Baada ya ziara ya Naibu waziri wa Kilimo Dr Mary Mwanjelwa kutembelea mikoa inayozalisha zao la korosho, serikali imekiagiza chuo cha utafiti cha Naliendele kutafuta suluhu ya kudumu ya ugonjwa wa mnyauko fusari unaoyapata mazao ya korosho.
Naibu waziri Dr Mary Mwanjelwa ameomba utafiti huo ufanyike na kuja na suluhushi sahihi ili kuondoa ugonjwa wa mnyauko fusari ambao unaweza kusababisha kutoweka kwa zao la korosho nchini na kuhitajika kupatiwa ufumbuzi wa haraka.
Dr Mary akiwa mkoani Lindi ametembelea mashamba mbalimbali ya korosho ikiwemo shamba la Benki ya korosho ya chuo cha utafiti cha Naliendele na kujionea miti ya korosho iliyopandwa toka 1958 na bado inaendelea kuzaa mazo vizuri.
Comments