SUPER STAA wa muziki Duniani kutoka nchini Marekani, Beyonce amenunua jengo la Kanisa Kongwe mjini New Orleans nchini Marekani ikiwa ni harakati zake kujitanua na kueneza dini yake ya Beyism.
Kanisa hilo lenye zaidi ya miaka 100 limejengwa kwa mawe miaka ya 1900’s limemgharimu Beyonce kiasi cha dola $850,000 sawa na Tsh bilioni 1.9 kulinunua.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka mitandao mbalimbali ya burudani duniani ikiwemo TMZ, Jezebel, papermag.com, Shaderoom na nyingine zinaeleza kuwa, lengo la kununua kanisa hilo ni kueneza dini yake ya Beyism na kuongeza waumini kutoka sehemu mbalimbali za dunia.
Beyism ni dini ambayo wafuasi wake wanamsujudu Beyonce kama ‘mungu’ wao na tayari imeshapata maelfu ya waumini nchini humo
Mwaka 2014, waumini wa dini ya Beyism walianzisha kanisa la rasmi la Beyonce walilolipa jina la ‘The National Church of Bey’ mjini Atlanta nchini Marekani.
Waumini wa Kanisa hilo wanaimba nyimbo za Beyonce na kusoma biblia maalumu zinazoitwa beyble.
Kanisa hilo limepambwa na picha nzuri za Beyonce akiwa amevalia mavazi ya nguo kama za viongozi wengine wa makanisa ya kikristo.
Kanisa hilo lenye ukubwa wa eneo la square futi 7,500, lina vitanda viwili, mabafu mawili.
Comments