RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

Ambwene Mwasongwe asema “haya maneno ni mazito sana hasa kwetu vijana”

Muimbaji Wa Muziki Wa Injili Tanzania Ambwene Mwasongwe ambaye licha ya kufikisha ujumbe wake kwa njia ya nyimbo pia hutumia mitandao ya kijamii kuwafundisha mashabiki zake mambo mbalimbali ya kiroho na hata kimaisha.


Kupitia ukurasa wake wa facebook leo amezungumzia sana kuhusu madhabahu na ameandika hivi;

“Moja ya maneno nayoyakumbuka na naambiwa Mara kwa Mara na wachungaji wangu, na watumishi wa Mungu, ni KUHESHIMU SANA USAFI WA MADHABAHU.

Nanukuu ” madhabahu hizi zinaombewa sana, wachungaji hawalali wanakesha na kugaragara kumtafuta Mungu KWA ajili ya kuandaa ibada, ukiingia na uchafu na ukawa vibaya utaharibiwa na nguvu ya madhabahu maana itakutema nje kabisa” Haya maneno ni mazito sana hasa kwetu vijana tuliopata Neema ya kusimama na kuingia madhabahu za kila aina
Lazima tuwe tuna ibada binafsi na Mungu ili kutumika kwa uaminifu zaidi.”



“Popote unaposoma ujumbe huu, kama wewe ni mtumishi wa madhabahu chukua maonyo ambayo nami huwa napewa ( hasa sisi waimbaji) maana tunasimama madhabahu nyingi sana, USALAMA NA PONA YETU NI KUKAA NDANI YA YESU KWA UAMINIFU, ILI KAMA MADHABAHU NI YA HOVYO KUSIMAMA KWAKO KUKAIBOMOE NA KAMA NI SAFI NA TAKATIFU BASI IKAKUSAIDIE KUHUDUMU KWA VIWANGO VYA USAFI, kinyume na hapo ni maumivu makali. Mungu atusaidie”

Comments