Dr Msowoya aja na *Tumaini Campaign na J6* -Awapa wanafunzi wa kike mbinu kumi za kutimiza ndoto zao
Na Mwandishi wetu, Iringa
Mwenyekiti wa Umoja wa Waimbaji wa Muziki
wa Injili, Mkoani Iringa ambaye ni mwanaharakati wa haki za watoto na
wanawake, Dr Tumaini Msowoya ameanzisha *Tumaini Campaign* inayolenga
kuhamasisha watoto wa kike wasome kwa bidii na kutimiza ndoto zao.
Kupitia kampeni hiyo amewapa wanafunzi wa kike mbinu kumi zitakasowasaidia kufikia ndoto zao.
Dr Msowoya alikuwa akizungumza na wanzfunzi wa kike zaidi ya 200
wa Ifunda Tech kupitia kampeni yake ya *Tumaini Compain* inayolenga
kupambana na changamoto zinazozuia watoto wa kike kushindwa kualiza
masomo.
Dk Msowoya alisema ni lazima wawe na malengo ya kufaulu masomo yao, wachukue hatua ya kusoma , wazingatie J6 na kuwa na nidhamu.
J6
ni Jitambue, Jiamini, Jikubali, Jithamini, Jipende, Jisamehe ulipokosea
na Songa Mbele ikiwa ndio ujumbe uliobebwa kwenye kampeni hiyo.
Mambo
mengine ni usafi, kuachana na makundi ya kijinga, kuwa na bidii katika
masomo, kujifunza elimu ya maisha kwa kusoma vitabu, makala mbalimbali
na kufuatilia historia za wanawake waliofanikiwa akiwamo Rais wa
Tanzania, Mh Samia Suluhu.
“Nina imani binti akijiamini, akajitambua,
akajithamini, akajikubali anaweza kufika mbali sana. Natamani kuona
wasichana wanaoanza darasa la kwanza wanamaliza chuo kikuu bila mmoja
wao kuacha masomo kwa sababu yoyote ile,” amesema Dr Msowoya.
Katika kampeni hiyo, Tumaini amekuwa akigawa taulo za kike shuleni.







Comments