PICHA ZA UVAMIZI WA ENEO LA RUMAFRICA LA RULEA SANGA BAGAMOYO BARABARA YA SADAN NATIONAL PARK ENEO LA BWAMAGA LAZABE
Mkurugenzi wa Rumafrica Rulea Sanga nilimpigia simu rafiki yangu Samweli (mjumbe kwa sasa) kuhusu maendeleo ya eneo langu kama liko salama. Naye alianza kunipongeza kuwa eneo langu anaona kuna watu wanaendelea na ujenzi na swameshafikia kozi ya nne ya totali za msingi karibu na mwisho wa shamba langu. Nikamjibu, "Sio mimi ninayejenga, na ndo nasikia habari hizi kwako." Akasema "Ndivyo ilivyo."
Nikamuomba aniulizie ni nani aliyeuza shamba langu la eka 2 bila ya mimi kupata taarifa yoyote. Samweli akanikubalia kunisaidia kwasababu yeye anaishi karibu na eneo langu Bagamoyo na alikuwa ananisaidia kulifanyia usafi kwa kukata majani na miti kuondoa msitu, na pia ameshawahi kufanya shughuli za kilimo kwa kupanda miwa, mihogo na haikuishia hapo na ndiye aliyehusika kuweka bimu za mipaka ya shamba langu la eka 2.
Mkurugenzi wa Rumafrica Rulea Sanga
Nikamuomba aniulizie ni nani aliyeuza shamba langu la eka 2 bila ya mimi kupata taarifa yoyote. Samweli akanikubalia kunisaidia kwasababu yeye anaishi karibu na eneo langu Bagamoyo na alikuwa ananisaidia kulifanyia usafi kwa kukata majani na miti kuondoa msitu, na pia ameshawahi kufanya shughuli za kilimo kwa kupanda miwa, mihogo na haikuishia hapo na ndiye aliyehusika kuweka bimu za mipaka ya shamba langu la eka 2.
Baada ya siku moja nikampigia simu Samweli kuulizia kama alimpata aliyeuza shamba langu. Alinijibu Samweli kuwa amempata (na sitamtaja hapa kutokana na sheria za kimtandao).
Siku ya Jumamosi 24.10.2025 Nikita Masaki Kilimanyege kufuatilia Mac yangu iliyoharibika Power Supplier katika kampuni ya Elite Computer kwa Mr. Aron mida ya saa 7:16 mchana nilipompigia aliyeuza shamba langu mazungumzo hayakuwa rafiki kabisa, akawa anadai ni nani aliyenipa namba yake bila ya taarifa. Mzozo ukawa ni mkubwa sana, nikamuomba nikutane naye Bagamoyo maana mimi naishi Tegeta Dar es Salaam. Akanijibu, "Hawezi kuonana na mimi peke yangu mpaka niwepo na mtu aliyetoa namba yake, aliyeniuzia shamba ambaye ni Mr. Mnyalu ambaye alikuwa kama dalali ila mmiliki wa shamba hilo ni Masoud. Nikamwambia "Sawa".
Siku ya Jumamosi 25. 10. 2025 nilifunga safari kutoka Dar es Salaam mpaka Bagamoyo. Nilipofika mahali pale nilimpigia simu Samweli na kumjulisha kuwa nipo Shambani na sasa naelekea kwa Balozi. Samweli alinijibu kuwa "Yuko naye balozi kanisani, ikiisha Ibada tukutane sote nyumbani kwake."
Baada ya muda mfupi nilikutana na Balozi Kennedy na kusalimiana naye kujitambulisha kwake na kumueleza jinsi nilivyopata taarifa kutoka kwa Samweli za uvamizi wa shamba langu. Balozi akaniambia kwa hapa nyumbani kwake hana jibu la kutoa ila twende eneo la tukio halafu tukayajadili huko.
Tulipofika eneo la tukio nilimuonyesha mipaka ya shamba langu la eka 2 na zile bimu pamoja na majirani zangu. Balozi Kennedy akaniambia, amenisikia ila kuna vitu vilifanyika mpakaa hili eneo langu likagawiwa kwa huyo anayejenga au mvamizi wa ene langu. Sababu alizozitoa:-
1. Eneo halijaendelezwa kwa muda mrefu na kulikuwa na chaka kubwa au pori.
2. Katika vikao vyao walijadili kuwa mtu asipoendeleza shamba lake kwa miezi mitatu ligawiwa kwa mtu mwingine mwenye uhitaji na atahitajika kuchangia Tshs. 40,000 kwa eka Pia kuchangia ujenzi wa kisima cha kijiji pamoja na ujenzi wa shule kwa maendeleo ya kijiji.
3. Maeneo hayo huwa hayauzwi kwa sababu ni mali ya serikali na kumekuwa na mgogoro mkubwa kati ya wakazi wa kijijini hapo na serilikali kwa kipindi kirefu mpaka ikafika wakati wanakijiji wakapeleka malalamiko mahakamani na kwa mkuu wa mkoa au wilaya (Sina uhakika hapo).
3. Kuna vikao via Kijiji vilikuwa vinafanyika na kuchangiana michango (mkeka) kwaajili ya kesi na ujezi wa shule na kisima, mimi nilionekana kutohudhuria au kushiriki hata kakao kimoja wala kuchangia chochote. Niliwauliza ni njia gani walikuwa wanatumia kuwajulisha wanakijiji wanaokaa nje ya eneo hilo la Bagamoyo (shamba)? kwa maana mimi nilikuwa naishi Tegeta dar es Salaam na nilikuwa sipati taarifa hizo kwa miaka 7 sasa. Akasema kuna "group" na mawasiliano mengine yalikuwa yakifanyika kuwajulisha ila mimi taarifa zangu zilikuwa hazipo kwenye orodha ya wanakijiji hao." Nikamjibu, "Mimi sikujua hilo na nilikuwa sijui Kabila kuwa kuna taratibu hizo kwa miaka yote 7 yote."
Kwahiyo Balozi Kennedy akaniambia kuna vitu viwili vinaweza kunisaidia ili nisipoteze kabisa eneo langula eka 2 na gharama nilizotumia katika ununuzi na kutunza eneo hilo kwa kulifanyia usai wa kukata majani, visiki na miti kwa muda wa miaka 7:-
1. Wanitafutie eneo lingine nje na hapa barabarani lilipo shamba langu kwa sasa. Nilipie Tshs. 80,000 kwa ukubwa wa eka 2 na niliendeleze ndani ya miezi mitatu kwa kujenga nyumba au kufanya shughuli za kiuchumi.
2. Na mimi nilete matofali na kuanza kujenga katika eneo hilo ili atakapokuja huyo mvamizi tuwezi kutafuta suluhisho. Kwasababu aliyeuza hilo eneo alipopigiwa simu ya Balozi Kennedy kuomba namba ya simu ya mvamizi kama nilivyomuomba, akasema, "Hawezi kutoa namba hiyo ya simu."
Baada ya kusikia taratibu hizo nilimjibu. "Kabla sijaamua kupelekwa eneo jingine natamani nikutane na aliyevamia eneo langu nimueleze kuwa mimi ndiye mmiliki halali wa eneo hilo tangia 2018 kwahiyo asimamishe ujenzi wake ili tupate muafaka.
Kwa maamuzi yangu yaharaka nikamwambia Balozi Kennedy tutakavyoongea na aliyevamia eneo hilo na kuona kunauelewano mzuri basi amege eneo na mimi niwe na mji katiika eneo la barabarani. Au alipe gharama zangu za uendeshaji wa ene hilo. Ikiwa ngumu basi nitaona cha kufanya ikiwa ni pamoja na kwenda kwenye hilo eneo jingine au kumuachia Mungu wa haki atende haki yake. Akanijibu Balozi Kennedy "Ni sawa kwa maanuzi yako ila uwezekanao wa kumuondoa huyu mvamizi kwa sasa ni ngumu kwasababu kishaanza ujenzi wake na kuna gharama amezitumia." Nikamjibu na mimi kuna gharama kubwa sana nimetumia kulitunza hilo eneo mpaka Leo hili mvamizi analikuta na kuanza ujenzi wake.
Katika maongezi engine akaniambia kuna watu wanne wameuziwa ene hilo hilo, na mwingine aliuziwa Tshs. 1,500,000 kwahiyo eneo hilo linaonekaa lina watu watano wanaomililiki.
Kikao chetu kilimalizika mida ya saa 8 usiku hapo shambani na baadae tukafunga kikao kwa kuwekeana utaratibu wa Balozi Kennedykunitafutia waliovamia shamba langu na nikamuahidi kurudi tena. Niliomba ridhaa kwake ya mimi kufanya Ibada Fuji katika eneo langu naye akaniruhusu.
Siku ya Juatatu 26.10. 2025 nilimpigia simu Balozi Kennedy ili kujua maendeleo juu ya suala langu la shamba alisema, "Bado hajafanikiwa kumpata aliyevamia. Akasema, "Kumpata mmiliki ni ngumu ila atajitahidi kumtafuta na itachukua muda mrefu sana kumpata. Nilipomuuliza ujenzi unaendeleaje? Akaniambia kwa sasa upo kwenye madirisha. Nilipomuomba aongee na wanaojenga eneo hilo ili apate namba za mvamizi akaniambia itakuwa ngumu kwa maana wao wapo kwa kujenga na hawataruhusu namba ya bosi wao. Akasema, ni ngumu wao kutoa namba za bosi wao kupewa mtu mwingine hasa kwa suala kama hili. Nikamwambia azidi kunitafutia hiyo namba ya simu maana yeye ndiye kiongozi wetu wa kusuluhisha mataizo kama haya kwenye kijiji chetu. Akasema "sawa." Nami nikamuahidi kuurde tena bagamoyo ili nikutane na mvamizi au mafundi wanaojenga eneo hilo ili nipple mamba zoo ikiwezekana wiki hit Ijumaa nitafika shaman kukutana na mvamizi na ikiwezekana wanaojenga ili nipple ushirikiano wao. Na nikamwambia mimi Bado Ninatambua Kuwa Eneo Hilo ni Langu.




Comments