RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION


BEATRICE DAVID MWENDAPOLE
Ni Dada ambae ukikutana nae uwezi amini kuna changamoto/Majaribu,Shida na taabu alipita.Beatrice ni Mama mwenye watoto wawili wakubwa alio zaa akiwa na umri wamiaka 18.Mwaka 1993 Mama yake mzazi alifariki Dunia na Baadae mwaka 1999 Baba yake mzazi alifariki.
Beatrice 

Baada ya wazazi kufariki alipitia shida yakuto kuelewana na Kaka yake Mkubwa ambae mpaka sasa awaongei pamoja.Wazazi wao waliwaacha wakiwa watatu,Mvulana mmoja na mabinti wa wili.Kuto kuelewana uko kulitokana na Kaka yake kutaka kuuza nyumba bila kuwashirikisha.

Ugomvi huu ulidumu kwa takribani kwa miaka 7.Lakini kupitia maombi ya Dada huyu alie amini mtetezi wa Maisha yake ni Mungu alipigana nakuakikisha nyumba haiuzwi.Ukiachilia mbali ugomvi wa Kaka yake,Maisha yalibadilika nakuwa magumu sana kwani kuna wakati alishindwa kuwalea watoto wake kutokana nakuto kuwa na kazi.

Lakini katika haliyote hiyo akuacha kumlilia Mungu awe mtetezi wa Maisha yake hasa watoto wake.Kuna wakati alilala njaa na watoto wake bila kupata msaada kwa ndugu yeyote.
Beatrice akifanya maojiano na Blogger Uncle Jimmy.


Anaendelea kueleza hali ya Maisha ilikuwa ngumu nakufikia sehemu yakutaka kukata tamaa yakuishi.Marafiki,Majirani,Ndugu walimtenga kisa wokovu.Mwaka 2010 akiwa katika hali hiyo alifanyikiwa kupata pesa kidogo aliokuwa akiipata katika kodi ya wapangaji walio wapangisha katika nyumba walio waachia Marehemu wazazi wake.
Ndipo Beatrice akapata wazo lakusomea uwandishi wa habari nakufanyikiwa kumaliza kozi iyo na sasa ni mwandishi katika Magazeti ya jamii.

Anakutia moyo ndugu msomaji akuna jambo gumu lakumshinda Mungu.Unapo pitia majaribu yoyote mwamini mungu ndie mtetezi wa Maisha yako

Comments

Anonymous said…
ttp://abdallahmrisho.blogspot.com/2007/10/mtangazaji-radio-one-hatunaye.html
DEMU AZUA KASHESHE MSIBANI!

Mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Beatrice Mwendapole, mkazi wa jijini Dar es Salaam,
katikati ya wiki hii alivamia msiba wa Mtangazaji wa Kituo cha Radio One na Televisheni cha ITV, Moses Justine na kudai alikuwa mchumba wa marehemu huyo.

Kitendo hicho, kiliwashangaza wengi miongoni mwao ni mama mzazi wa Moses na dada zake ambao walisema hawamtambui.
Akizungumza na Ijumaa, Beatrice alidai alishangazwa na kitendo cha mama mkwe na wifi zake kumkana wakati yeye na marehemu waliishi kama mke na mume kwa zaidi ya miaka miwili.

Beatrice alisema kinachomuuma ni kitendo cha ndugu wa Moses kumtimua na kumuambia akitaka kukaa pale msibani akae kama waombolezaji wengine lakini madai yake ya uchumba hawayatambui.
Huku akilia, mwanamke huyo alidai yeye ndiye aliyekuwa akimuuguza marehemu mpaka alipofariki Oktoba 10, mwaka huu katika Hospitali ya Dk. Kairuki, Mikocheni jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa wiki mbili.

Kufuatia madai hayo, mwandishi wetu alifanikiwa kuzungumza na mama mzazi wa Moses, Mary Justine ambaye alimkana mwanamke huyo.

Mama huyo alimtaja mwanamke mwingine aitwaye Isabela Massawe kuwa ndiye alikuwa mchumba wa marehemu mwanaye. "Kwa ujumla simtambui huyo dada Isabela anayejiita mchumba wa mwanangu," alisema mama Mary.

Mama huyo alisema mwanaye ameacha mtoto mmoja aitwaye Goodluck.

Naye dada wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Dora Justine, alisema; "sisi tunamshangaa huyu mwanamke anayejitangazia eti, yeye ndiye mchumba wa marehemu wakati wifi yetu aliyetuonyesha kaka ni Isabela, yeye wala hatumjui".

Marehemu alizaliwa mwaka 1965 kijiji cha Mkalama wilayani Iramba mkoani Singida na kusoma Shule ya Msingi Naura mwaka 1975 mpaka 1981 na hatimaye alipata elimu ya Sekondari katika Shule ya Enaboisho iliyopo Arusha na baadaye kupata kozi mbalimbali.