MTANGAZAJI WA PRAISE POWER, ERICK BRIGHTON KUACHANA NA UBACHELA MEI 2012
Ikiwa ni siku ya kwanza kuanza kikao cha harusi ya mtumishi wetu Brighton katika hotel ya The Atriums Sinza, wadau na wapenzi wa Erick Brighton wametokea kufurahishwa sana na uamuzi wa brother wetu.
Kikao cha kwanza tayari kimeshafanyika na kikao cha pili kitafanyika siku ya Jumatatu mida ya saa moja Mwenge.
Kamati ya maandalizi inakukaribisha sana kum-support Bwana Erick na kama wewe ni msiikilizaji wa Praise Power usikose. Kumbuka Brighton amefanyika baraka sana kwa wanakesha na Praise Power. Hapo chini kuna namba za simu kwaajili ya kujua tutakapokuwepo katika kikao cha pili. Mungu akubariki
Comments