RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

IGIZO LA YESU LATEKA HISIA ZA WATU JIJINI LONDON KATIKA IJUMAA KUU

Nikiwa kwenye pozi na mwigizaji mkuu mara baada ya igizo!

Igizo la kufa na kufufuka kwa Yesu lililoandaliwa na Wintershall charitable trust ya nchini Uingereza limekonga mioyo ya maelfu ya watu waliojazana katika uwanja wa wazi wa Trafalgar Square jijini London hapo jana baada ya waigizaji kufanikiwa kuigiza kwa kiwango cha juu na kufikisha ujumbe sawia uliopokelewa kwa shangwe za makofi na kelele nyingi.


Onyesho hilo la wazi linaloitwa ''The Passion of Jesus Trafalgar Square 2012, mwigizaji mkuu katika igizo hilo aliweza kuteka hisia za watazamaji kutokana na uigizaji wake makini,zaidi ni jinsi anavyofanana na mwigizaji mwingine aliyeigiza filamu ya Yesu bwana Brian Deacon ambaye gospel kitaa ilikuandikia habari yake hapo jana,Igizo hilo ambalo liliigizwa mara mbili hapo jana saa sita mchana pamoja na saa tisa na robo alasiri ambapo kwa watu walioshindwa kuona waigizaji moja kwa moja walifuatilia kupitia kioo kikubwa au projecror iliyokuwapo eneo hilo, pia lilihudhuriwa na askofu wa London kanisa Anglican Richards Chartres,ambaye alitoa shukurani zake kwa maelfu ya watu waliohudhuria onyesho hilo pia kwa charity ya wintershall kwa kuandaa onyesho hilo ambalo hufanyika kila mwaka katika eneo hilo.

                      ANGALIA BAADHI YA PICHA AMBAZO GK IMEFANIKIWA KUZIPATA









 Projector kubwa iliyokuwepo eneo hilo ambayo iliweza kuonekana hata kwa wapita njia na wasafiri barabarani.

Yesu baada ya kumaliza maombi bustani ya Gethsemane 

Yuda akiwa tayari kumbusu Yesu ili akamatwe.



Kaburi lakutengenezwa likiwa pembeni.

wakienda kuuzika mwili wa Yesu

shughuli za mazishi.

Yesu baada ya kufufuka(mwenye nguo nyeupe katikati)



Mwigizaji akiwa katika pozi mbalimbali na mashabiki wake.

Comments

Unknown said…
Hahahaaa! nafurahi kwa kuwa watu wa Uingereza walipata ujumbe kuhusu maisha ya Yesu. Hawa jamaa waigizaji hakika walifnya maandalizi makubwa sana na kwa kweli nawapongeza sana. Amina.