RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

NANI MSHAMBA? – STARA THOMAS


“Aliye kwa Yesu ni mjanja, Aliye kwa Yesu si mshamba, Yuko kwenye mwanga, mwanga wa milele”
Stara akiongea na moja ya redio ya Injili amesema baada ya yeye kumpa Yesu maisha yake “wengi walinitenga na wengine kunidharau lakini mimi sijali maana mtu anayekuwa kwa shetani ni mshamba”
Album ya dada Stara NANI NI MSHAMBA iko tayari na itasambazwa mwezi wa nne.

Habari nyingine zinazosikika ni kuhusu Beatrice William aliyepata umaarufu kupitia Bongo Star Search naye ameokoka tarehe 7/3/2012 kwenye kanisa la Mikocheni B Assemblies of God (Mlima wa moto)
Alipoongea akiwa madhabahuni tarehe 9 Machi kwenye mkesha kuhusu uamuzi wake wa kumpokea Bwana Yesu alisema “Ni uamuzi wangu wa dhati kuokoka na akili zangu timamu. Mara nyingi nilipenda sana kuokoka lakini niliogopa kumbipu Mungu kama wengine wanavyofanya”

Source: Strictly Gospel

Comments