NDUGU YETU PUMZIKA KWA AMANI STEVEN KANUMBA THE GREAT
Ni majonzi makubwa sana kwa Watanzania wote sisi tulimpenda lakini Mungu kampenda zaidi, inauma sana kwa kijana mdogo kama Kanumba kufariki wakati alikuwa bado hajazitima ndoto zake .Mungu ailaze roho ya marehemu Swaiba wangu Steven Kanumba ni mengi sana tuliyoyafanya mimi na wewe katika gurudumu ili la sanaa bila kujali yote yaliyotokea ni kawaida ya binadamu kutoelewana kama Baba na Mama wanafunga ndoa kanisani na wanakula viapo vya utii mbele za Mungu lakini wanagombana na kufikia hatua ya kuachana kwanini ishindikane kwetu ni hali ya kwaida katika maisha binadamu kutofautiana mengi yanazungumzwa juu yangu ila kila kitu mimi namuachia Mungu mimi ni mnyonge siwezi kupambana nanyi mnaoniongelea vibaya maumivu nayoyapata juu yenu Mungu hatowaacha siwezi kuzizuia hisia zenu kuzungumza yale mnayojisikia kuzungumza
Muda mfupi tu baada ya kufariki Steven Kanumba akiwa kwenye gari lake la kifahari Lexus tangulia ndugu yangu sisi tuko nyuma yako maana kila nafsi itaonja umauti. wadau nilikuwa kimya kwa kutowaletea matukio kwa sababu ya shughuli zilkuwa nyingi sana katika msiba nilikuwa kwenye kamati ya mazishi hivyo sikuwa nakipata muda wa kutosha na sio watu wanavyofikiria jamani hata kama kuna matatizo ndio katika maswala ya msiba hapana jamani mimi sijafikia hali hiyo yakuwa na roho ya kinyama namna hiyo
Hapa tukiutelemsha mwili wa marehemu katika hospital ya Muhimbili ni mtu wa kwanza kufika katika eneo la tukio
Safari yetu ya mwisho binadamu wote mara ya kwanza nilipofika walikataa kumpokea pale hospital mpaka wapate PF 3 ndipo nilipowasha gari na kwenda Salenda polisi na kuwapata askari watatu ndipo tukapata fursa ya kwenda kumpuzisha marehemu
Tukimfunika macho maana yalikuwa wazi kama anasinzia
Hapa akiongea jambo na baadhi ya wanakamati ya mazishi
The Greatest nikimsikiliza Rais
Comments