RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

NDUNGU ZANGU NA WADAU WA BLOG HII, BLOGGER WENU RULEA SANGA NAPENDA KUWAAGA KWA KIPINDI CHA WIKI MOJA NITAKUWA NIGERIA KWA NABII TB JOSHUA



Meneja Masoko Glorious Celebration na Blogger wa Blog hii, Rulea Sanga

Hatimaye safari yangu imefika ya kuelekea kwa Nabii TB Joshua. Safari yangu itaanza kesho saa 6:00 usiku siku ya Jumatano tarehe 18 Aprili 2012.

Mwaliko huu umetokana na Nabii TB Joshua kupendezewa na blog yangu ambayo mara nyingi huweka habari zake ambazo zimekuwa baraka kwa watu wengi ulimwenguni. Watu wengi wamekuwa wakinitumia "message na email" kuhusiana na wanavyobarikiwa na kazi ya mtumishi huyu.

Nakumbuka siku ya kwanza kupokea simu kutoka Nigeria, sikuamini maana ilikuwa ni muujiza kwangu. Nilipokea simu kutoka kwa dada mmoja ambaye alijitambulisha kuwa yeye anatokea Nigeria kwa Nabii Joshua.....na mahojiano yetu yalikuwa kama ifuatavyo na yalifanyika kwa lugha ya kiingereza:

Simu: Dreeeeeeeeeee
Rulea: Nikaiangalia namba na kuona namba inatoka nje ya Tanzania....Nikaipokea simu.....Hellooo
Dada kutoka Nigeria: Hello....Habari yako.

Rulea: Salama, Habari yako.

Dada kutoka Nigeria: Nzuri, napiga simu kutoka Nigeria kwa Nabii TB Joshua

Rulea: (Nakahisi kutetetemeka) .... Ndiyo dada yangu unasemaje?

Dada kutoka Nigeria: Kuna habari fulani tumeziona katika blog yako zinazomhusu TB Joshua, ni wewe umeziweka na kuziandika?

Rulea: (Niliogopa sana nikidhani labda nimeandika kitu kibaya) ....Nikamwambia ni kweli nimeziandika ila zingine nimechukua katika blog za watu wengine..

Dada kutoka Nigeria: Sasa Nabii TB Joshua anataka kuongea na wewe

Rulea: (Mhhhh..akili yangu ikawa inawaza kuwa ni matepeli wa Nigeria) .... Ok sawa.

Nabii TB Joshua: Hello...Habari yako.

Rulea: Nzuri, Bwana asifiwe?

Nabii TB Joshua: Ameni.....Nimependa kazi yako...natengependa nikualike SCOAN Nigeria....Natamani kukuona.

Rulea: Ahsante  sana..mimi niko tayari katika mwaliko wako.

Nabii TB Joshua: Endelea kuongea na huyo dada uliyekuwa unaongea naye

Rulea: Nashukuru..Mungu akubariki

Dada kutoka Nigeria: Samahani..wewe ni nani katika kikundi cha Glorious Celebration, kwani tumeona katika blog yako na tumekipenda kwa huduma zake.?

Rulea: Mimi ni meneja masoko na pia ndiye ninayeweka habari zao katika mitandao

Dada kutoka Nigeria: Mko wangapi katika kikundi chenu?

Rulea: Tupo kama watu kama 13

Dada kutoka Nigeria: Sasa si muda mrefu utapigiwa simu na "Cordinator" wetu aliyoko Tanzania, Dar es Salaam-Masaki anayeitwa Martha ili achukue habari zako na za kikundi cha Glorious Celebration.

Rulea: Sawa..nashukuru.

Dada kutoka Nigeria: Kwaheri ila tutakupigia tena

Baada ya muda mchache nikapokea simu kutoka kwa dada Martha aliyoko Tanzania.

Simu: Dreeeeeeeeee

Rulea: Hello

Martha: Habari yako...Ninaitwa Martha kutoka Masaki...ni cordinator wa kanisa la SCOAN Synagogue la Nabii TB Joshua wa Nigeria.

Rulea: Ndiyo dada yangu.

Martha: Umepokea simu yeyote kutoka Nigeria...

Rulea: Ndiyo:

Martha: Ninaomba kesho uje na baadhi ya viongozi wa Glorious Celebration Masaki.

Rulea: Sawa dada yangu nitafika.

Martha: Usiku mwema.

Rulea: Na wewe pia.

Baada ya muda mfupi nikainua simu yangu na kumpigia kiongozi wa muziki wa Glorious Celebration, Emmanuel Mabisa na kumwelekeza yaliyonikuta na kumweleza kesho tunatakiwa Masaki.

Siku ya pili ilipofika...tukafunga safari mpaka Masaki (walioenda ni Rulea, Emmanuel Mabisa na Chaka. Na tulipofika tukaulizwa maswali yanayohusiana na Historia fupi ya Glorious Celebration na uongozi wake. Na baada ya hapo kila mtu aliyefika mahali hapo akaanza kuulizwa "particulars" zake...na kila mtu akazitoa.

Baada ya kumaliza zoezi hilo tukaambiwa tutaitwa tena....Tulirudi majumbani kwetu na baada ya muda wa kama wiki moja hivi tukaitwa tena. Na kuelezwa ni watu wangapi wangeweza kwenda na vitu gani vya kufuata.....(Sitoweza kuelezea kila kitu mdau wangu)...Ila ningependa kukujulisha kwamba uongozi wa Nabii TB Joshua ulitoa namba ya watu kwenda nao...na ili-suggest kumchukua kiongozi mmoja wa Glorious Celebration, Emmanuel Mabisa kama muwakilishi wa kikundi

Kwa kumalizia tu, baada ya muda wa miezi miwili nikimaanisha Februali-Aprili niliitwa na dada Martha katika ofisi zao zilizoko Posta katika jengo la Benjamini Mkapa floor ya kwanza na kupewa fomu za kujaza kwaajili ya VISA. Nakumbuka kipindi kilikuwa kigumu sana kwangu kwani rafiki yangu Emmanuel Mabisa alikuwa katika maombi Chanika na Glorious Celebratoion kwaajili ya maandalizi ya Pasaka. Na nilipompigia simu kuwa wanahitaji passport yako..na yeye akasema yuko mbali na hataweza kufika kwa siku hiyo, na akaniamuru nibomoe ofisi yake na kutafuta hiyo passport..na mimi nilifanya hivyo.

Zoezi la ujazaji form ulipoisha niliambiwa tutapigiwa simu kujua soiku ya kuondoka na kuelekea Nigeria. Sikumbuki ni tarehe ngapi ila ni mwezi wa April nikatumiwa message ikinijulisha kuwa tarehe 8 April 2012 tunatakiwa kwenda ofisi za TB Joshua kwaajili ya maelekezo ya safari. Jumatatu 16 April  nikiwa Arusha katika Uzinduzi wa Albamu ya Ruach Waorship Team nikatumiwa message kuwa tarehe 17 April natakiwa asubuhi kuwa katika ofisi za TB Joshua-Tanzania kupewa maelekezo ya safari ya tarehe 18...na mimi nilimjibu kuwa itakuwa ngumu kufika kwani hiyo tarehe ndiyo tarehe ambayo nitakuwa natoka Arusha kwahiyo nikifika Dar ges Salaam nitakufuata....Na dada Martha akanijibu kuwa basi tutaonana Airport saa sita usiku

Hayo ndiyo maelezo ya safari yetu ya kulelea kwa Nabii TB Joshua..Na sasa tunasubiria kuondoka 18 Aprili usiku wa saa sita


TUNAOMBA MAOMBEZI YAKO TUFIKE SALAMA NA TURUDI SALAMA