STEVEN KANUMBA AFARIKI DUNIA
Muigizaji wa filamu nchini Stephen Kanumba amefariki usiku wa kuamkia leo,baada ya ugomvi na mpenzi wake huko nyumbani kwake Sinza Vatican.Mpenzi huyo ametoroka na inadaiwa alimsukuma marehemu kwa nyuma na kudondokea kisogo.Kanumba alilalamika maumivu makali ya kichwa ambapo alimwuita mdogo wake ampeleke hospitali,lakini alifariki kabla hajafika huko.Mwili wake umehifadhiwa Muhimbili.Source: Radio One
Mkurugenzi wa Global Publisher, Erick Shigongo akishirikiana na watengenezaji wa hema.
Ndani ya geti la marehemu Steven Kanumba
Blogger Rulea Sanga aliyevalia njano halkukosa msibani
Mkurugenzi wa Global Publisher, Erick Shigongo akishirikiana na watengenezaji wa hema.
Ndani ya geti la marehemu Steven Kanumba
Blogger Rulea Sanga aliyevalia njano halkukosa msibani
H-BABA akihojiwa na waandishi wa habari
Wapenzi na ndugu wa marehemu Steven Kanumba nyumbani kwake
Mwigizaji Mainda wa pili kutoka kushoto akimfariji rafiki yake
Waigizaji wa filamu
Mwimbaji huyu alielezea jinsi alivyoaagana na Marehemu Steve Kanuba alipohudhuria katika bendi yake siku ya jana usiku, anasema marehemu alimtania kuwa kesho ambayo ni leo kuwa atakuja na suti kali sana ambayo ameinunua katika bendi yake
Mjasiliamali Shigongo wa Global Publisher akihojiwa na waandishi wa habari, alisema ni kitu chema kufanya kazi yako kwa kumkumbuka Mungu
Ruge wa Clouds FM alisema, ni pengo kubwa sana kwani katika sanaa alikuwa anahitajika sana
HISTORIA FUPI YA MAREHEMU STEVEN KANUMBA

HISTORIA YAKE:
Steven Charles Kanumbaa alizaliwa Januari 8, mwaka 1984 mkoani Shinyanga kabla ya umauti kumfiia Aprili 6, mwaka 2012.
Elimu ya msingi alipata katika shule ya Bugoyi, na baadaye akajiunga na sekondari ya Mwadui, kabla ya kuhamia Dar Christian Seminary.
Baada ya kumaliza Kidato cha Nne Dar Christian, Kanumba alijiunga na sekondari ya Jitegemee, Dar es Salaam pia kwa elimu ya Kidato cha Tano na Sita.
Ni ni wakati huo akiwa Jitegemee Kanumba alianza shughuli za sanaa katika Kundi la Kaole Sanaa Group la Magomeni, Dar es Salaam.
Baada ya kukomaa Kaole, Kanumba aliamua kuanzisha kampuni yake mwenyewe ya filamu na hadi anakutwa na umauti alikuwa mwigizaji anayefahamika Afrika nzima.
Ameshirikiana na wasanii wakubwa duniani kama Ramsey Nouah wa Nigeria na amefanya kazi na mastaa wengine kadhaa wa Nigeria.
Miongoni mwa filamu ambazo alifanya ni Dar To Lagos, She is My Sister, Ancle JJ, Oprah, Tufani, Johari, Gharika, Baragumu, Sikitiko Langu, Dangerous Desire, Cross My Sin, Village Pastor, Family Tears na kadhalika.
Hivi karibuni, alikaririwa akisema atagombea Ubunge katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.
Kanumba atakumbukwa na wengi sana kwa ucheshi wake- upole na ushirikiano mzuri na wenzake katika kazi.
Kifo cha Kanumba ni pigo katika tasniya ya filamu Tanzania. Taifa limempoteza mtu ambaye alikwishaanza kuitangaza vema nchi kupitia sanaa hiyo na ambaye angetarajiwa kuitangaza zaidi katika anga za kimataifa zaidi kupitia sanaa hii.
Nigeria sasa wanajua Tanzania sasa filamu. Nchi nyingi za Afrika zinajua sasa nah ii sehemu ya kazi nzuri kwa Kanumba.
Mwenyewe aliwahi kukaririwa alifika hadi Hollywood hadi Marekani, ambayo ni ‘makka’ ya wacheza filamu. Kwa sasa mwili wa marehemu upo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.
Mungu aiweke pema peponi roho ya marehemu. Amin.
Comments