RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

UTOTO WA KIROHO UNAZUIA MAFANIKIO YAKO, HUWEZI KUPATA BARAKA WAKATI HUTAKI KUKUA APOSTLE NDEGI

LIVING WATER CENTER BIBLE FELLOWSHIP
Apostle Onesmo Ndegi wa Living water.
                                        
Apostle Onesmo Ndegi ambaye ni mchungaji kiongozi wa kanisa la Living water Tanzania lenye makao makuu yake Kawe jijini Dar es salaam,ameendelea kufundisha somo la  namna ya kufanikiwa kimaisha kupitia kipindi chake cha ''KWELI IWEKAYO HURU'' kinachorushwa kupitia kituo cha Wapo Radio Fm ya jijini Dar es salaam kila siku za ijumaa kuanzia saa nne kamili usiku.

Katika mwendelezo wa somo hilo ambalo wiki moja nyuma alifundisha juu ya Njia sahihi ya kufanikiwa kwetu, Ijumaa iliyopita aliendelea na somo hilo akifundisha kuhusiana na vizuizi vya mafanikio kama mkristo.Akishirikiana na mtangazaji wa radio hiyo Ritha Chuwalo,Apostle Ndegi alisoma neno kutoka kitabu cha wagalatia 4;1-2 mlango ambao unazungumzia juu ya urithi

''Tumetangaziwa urithi lakini pia kuna kizuizi,na kizuizi chenyewe ni utoto,na utoto wenyewe sio wa kimwili bali ni wa kiroho'' akatolea mfano wa mtoto ambaye amefiwa na wazazi wake kwamba hawezi kukabidhiwa urithi wake mpaka pale ambapo atakuwa amekua na kuwa na akili timamu isiyokuwa na shida ili aweze kuzimiliki na kuendesha vyema vivyo hivyo hata kwa Mungu wetu usipokuwa kiroho huwezi kumiliki yale yote uliyoahidiwa na Mungu,Waefeso 4;13-15

''Mungu anaangalia ni kwa jinsi gani ulivyofanikiwa kiroho, na ili uweze kukua  kuna kanuni za kufuata,kwanza unatakiwe ukue,ili upate kuongezeka ufahamu  wa kimungu'' akatolea mfano wa Yesu ambaye alikua na kisha kuianza kazi aliyotumwa.
akasoma neno '' Sio kiwango cha Askofu,Nabii au cheo chochote kile bali kinachotakiwa ni kukua kufikia kiwango cha Kristo,huwezi kutaka baraka wakati hutaki kukua''.Luka 2;52

Akizungumzia suala la watu kumuomba Mungu kwa kukariri maandiko amesema'' huwezi kufanikiwa kwa kumuomba kwa kukariri neno unachotakiwa ni kulijua neno na roho ndio dira ya mafanikio yako,usiombe kwa kukariri kwenye kitabu bali litoke ndani yako''.

Apostle Ndegi anaendelea na somo Ijumaa usiku kuanzia saa nne kamili usiku kupitia Wapo Radio Fm ambayo pia kama uko nje ya Tanzania unaweza kusikiliza kupitia ndani ya blog hii.Pia kila jumamosi kuna fanyika maombi maalumu kanisani Living water makuti Kawe kuanzia saa nne asubuhi.
Apostle Ndegi akiwafanyia maombi watu wenye mahitaji mbalimbali.
                          
TAZAMA VIDEO YA LIVING WATER MAKUTI KAWE PRAISE & WORSHIP MOJA YA WIMBO ULIOMO KWENYE ALBUM YAO YA KWANZA.

Comments