FLORA MBASHA AREJEA NCHINI AKITOKEA MAREKANI, KUIMBA KWENYE MKUTANO JANGWANI
Flora Mbasha akiimba kwahisia katika moja ya tukio nchini Marekani.
Baada ya ziara ndefu huko nchini Marekani mwimbaji nyota wa gospel
nchini Flora Mbasha pamoja na mumewe wamerejea nchini. Waimbaji hao
walikwenda nchini Marekani toka mwezi March mwaka huu na kufanikiwa
kuimba katika makanisa na mikusanyiko ya watu wa Mungu pamoja na semina
ya mwalimu Christopher Mwakasege.''
Bwana
Yesu asifiwe sana. napenda kuwashukuru wote kwa maombi yenu na
ushirikiano wenu kwa kipindi chote tulichokuwa Marekani kwenye huduma,
sasa tumerudi Tanzania salama kabisa. Mungu awabariki sana tunawapenda
naomba tuzidi kuwasiliana, kushauriana na kutiana moyo katika safari
yetu ya kwenda mbinguni. Amen
Pia waliweza kutembelea ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na kukutana
na watanzania wanaoishi nchini humo, Flora Mbasha anayetamba na matoleo
mbalimbali ya muziki aliweza kujitambulisha vyema katika tasnia hiyo
alipotoa wimbo Tanzania uliotoa hamasa kwa waimbaji wengine zikiwemo
kwaya kuimba juu ya Tanzania, pia wimbo wa Jipe moyo,Kila jambo,Yatima,
wimbo wa maisha ya ndoa aliomshirikisha mumewe Emmanuel Mbasha pamoja
na wimbo wenye mahadhi ya watu wa mikoa ya Pwani uitwao Mwanamke simama
imara.
Kwasasa mwimbaji huyo anamiliki studio yake mwenyewe ya kurekodia
iliyopo Tabata anakoishi pamoja na kuwa na matoleo ya audio na video
zaidi ya mbili, mwimbaji huyu ni mmoja kati ya waimbaji wanaomtukuza
Mungu katika mkutano mkubwa wa injili uitwao June Crusade unaoendelea
katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es salaam ukitarajiwa kuhitimika
jumapili hii huku mnenaji mkubwa akiwa ni askofu mkuu wa E.A.GT. Dkt.
Moses Kulola ambaye ni babu wa mwimbaji huyo. Karibu nyumbani Flora na
Emmanuel Mbasha asanteni kwa kutuwakilisha unyamwezeni.
ANGALIA BAADHI YA PICHA ZA MATUKIO YAO NCHINI MAREKANI
Walitembelea Sauti ya America kitengo cha Kiswahili kama unavyowaona.
Akiwa na balozi Mh. Mwanaidi Majaar alipomtembelea ofisini kwake.
Story zikiwa zimenoga mwe
Mbasha akitoa darasa la kucheza mwe style ya pikipiki kama sio baiskeli.
Weee Mbasha wewe haya tuambie hiyo ni key gani mwe
Flora aliweza kusherehekea sikukuu yake ya kuzaliwa nchini Marekani, hapa akiwa na keki yake.
Comments