RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MKURUGENZI WA RUMAAFRICA, RULEA SANGA AFANYA MAHOJIANO NA MTANGAZAJI WA RADIO YA KIKRISTO MJINI MBEYA DARAJANI - USHINDI RADIO KUHUSIANA NA MATUMIZI YA MITANDAO (BLOGS NA TOVUTI) SIKU YA ALHAMISI

Mwezi June 2012 ilikuwa ni siku ambayo nilialikwa katika radio ushindi FM iliyoko Mbeya kwa mahojiano na mtangazaji Fredy katika kipindi chake cha Super Mix. Mahojiano yetu yalihusiana na mitandao kama vile blogu na tovuti (website)

katika kipindi hicho huwa kunakuwa na mpambanisho wa wageni wawili, na mimi nilipambanishwa na Angel Bernard ambaye ni mwimbaji wa nyimbo za injili wa kikundi cha Glorious Celebration. Katika mpambano huo, Angel Bernard alionekana upendwa sana na wasikilizaji wa Ushindi Radio.

Nilichogungua ni kwamba maada yangu ilikuwa ngeni kidogo kwa watu waliowengi. Ndio maana watu wakawa wanamwelewa vizuri Angel kwani yeye alielezea sana kazi ya muziki na biashara zake. Kumbuka Mbeya ni mji ambao unapenda sana suala la uimbaji....Haya ndiyo niliyoyaona kama blogger.

Tunahitaji mablogger kusambaza sana elimu ya blogu kwa wapendwa ili waweze kufaidika katika huduma ya Mungu na katika biashara zao.


Mtangazji wa Radio Ushindi FM, Fredy
Mkurugenzi wa RUMAAFRICA, Rulea Sanga
Fredy akiwa busy kuhakikisha watu wanapiga simu-LIVE
Mchungaji Mathew akimhoji mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka katika kikundi cha Glorious Celebration kuhusiana na uimbaji wake.

Hapa ilikuwa katika mapumziko, ngoma za Mungu zikipigwa
Fredy akipokea simu za wasikilizaji
Kazi inasonga


Mchungaji Mathew Sasali akimpiga swali Angel Bernard kwa njia ya simu. Angel wakati huo alikuwa Dar es Salaam




Fredy akiwa ameweka simu katika kipaza kwa lengo la wasikilizaji kusikia sauti kutoka kwa Angel Benard aliyoko Da re Salaam




Nikitokelezea




Hekima ilihitajika sana siku hiyo kutokana na maswali kutoka kwa Fredy












Comments