RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI ASHINDA URAISI WA SHIRIKISHO LA MUZIKI TANZANIA
 
Addo November na binti yake

Mwanamuziki Wa Injili Tanzania Addo November Mwasongwe ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Muziki wa Injili Tanzania ameshinda katika Uchaguzi wa Kutafuta Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania inayoundwa na (CHAMUHADA, TAFOMA, INJILI, KIZAZI KIPYA, ASILI, DISCO).
November ameteuliwa Kuwa Rais Wa Mashirikisho hayo Tanzania. Uchaguzi huo Uliofanyika BASATA mchana huu umempa Ushindi wa Kishindo Muimbaji huyo wa Injili.

Addo November Amewashinda Washiriki wengine wa Kinyang’anyiro hicho wanne Abdul Elsavador, Mkoloni (Tanga Kunani) na Samuel Semkuruto ambapo Addo alipata Kura 8 Mkoloni Semkuruto Kura 4 na Elsavador Kura 4. Uchaguzi huo Uliomalizika Mchana huu saa 7:40 Unamfanya Addo November kuwa Rais Wa mashirikisho hayo kwa Muda wa Miaka 3 Mfululizo.

Addo November ni Mwanamuziki wa Injili anayetamba na Albam yake ya “Utabaki Kuwa Mungu”, Ni Baba wa Watoto Wawili na Mke Mmoja, Ni Mwanasheria (Advocate) na Sasa ni Mwajiriwa pia Wa Taasisi Moja Nyeti Ya Serikali Kama Mwanasheria wa Taasisi hiyo ya Fedha hapa Tanzania.

Addo alipochukua fomu za kugombea kiti cha ubunge jimbo la Iringa mjini kwa tiketi ya CCM, 2010

Comments