RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

REBECCA MALOPE KUTOA ALBUM YA NYIMBO ZA KIINGEREZA PAMOJA NA TENZI HIVI KARIBUNI.

Rebecca Malope akiimba wakati wa tamasha la pasaka jijini Dar es salaam mwaka huu.

Malkia wa muziki wa gospel barani Afrika bi Rebecca Malope ameweka bayana kwamba yupo kwenye mchakato wa kurekodi album maalum ambayo itakuwa ya nyimbo za kiingereza pekee, ambapo mpaka sasa kupitia kampuni yake ya muziki mchakato wa kuandaa album hiyo tayari umeanza.

Mwimbaji huyo aliyepata mafanikio makubwa katika tasnia ya muziki wa gospel tayari ana album 33 za audio ikiwemo mpya aliyorekodi mapema mwezi wa pili mwaka huu akiwashirikisha Tshwane Gospel Choir, ambayo kwa upande wa DVD itakuwa ya 5 lakini ya kwanza kurekodiwa live. Rebecca ameweka wazi mpango wake huo wakurekodi album maalumu ya nyimbo za kiingereza wakati akihojiwa kupitia kipindi cha runinga cha Expresso kinachorushwa na Sbc3.

Mwimbaji huyo pia ameweka bayana kwamba anatarajia kutoa kitabu cha nyimbo zake za tenzi( ama album) kwa lugha mbalimbali nakuwataka mashabiki wake na wapenzi wa gospel kwa ujumla kukaa mkao wa kupokea album hiyo pamoja na kitabu.Rebecca amekuwa akitoa nyimbo kwa lugha ya nyumbani kwao lakini pia amekuwa mda mwingine akiweka wimbo mmoja wa kiingereza katika album zake, hata hivyo hakuweka bayana kama nyimbo katika album hiyo itakuwa mpya tupu ama atachanganya na za zamani.

Akizungumzia majaribu mwimbaji huyo amesema kabla ya kushinda kinyang'anyiro cha uimbaji alikuwa na album tayari ya gospel ambayo aliirekodi na kwaya kanisani kwao alipoipeleka kwa kampuni ya muziki na usambazaji walimkatalia hali iliyomfanya kurekodi album nyingine isiyokuwa ya gospel nakujikuta kampuni hiyo ikimkubalia kuingia naye mkataba lakini anasema tayari Mungu alishamchagua kumtumikia hivyo kampuni hiyo ikamtaka mwimbaji huyo kuendelea na uimbaji wa gospel.

Majaribu mengine ni pamoja na wakati ameingia jijini Johannesburg pamoja na marehemu dada yake anasema maisha yalikuwa magumu sana alikuwa akizungukia makampuni ya kwenda kuingia nayo mkataba wa uimbaji lakini yalikuwa yakimtolea nje mpaka alipofanikiwa na Mungu kuendelea kumpigia mpaka sasa akiwa mwenye mafanikio. Mwimbaji huyo alibariki wengi alipokuwa nchini kwa mwaliko wa kampuni ya Msama Promotions wakati wa tamasha la pasaka katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam, bofya hapa kutazama matukio yake.




Rebecca Malope katikati akizungumza ndani ya Wapo Radio Fm alipofika kwa mahojiano kuhusiana na tamasha la Pasaka, kushoto kwake Ai Laizer mtangazaji wa Wapo na kulia kwake ni Elie John mtangazaji na fundi mitambo wa WAPO Radio FM. Ukitaka kuona picha za sauti na za mnato zaidi za tukio hili bofya hapa.





Comments