RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

WAIMBAJI WA ''KWETU PAZURI'' KUTUA UWANJA WA NDEGE JIJINI DAR ES SALAAM ALASIRI HII

Sarah Uwera mmoja wa waimbaji wa kundi hilo, walipotembelea nchini mwaka jana.
Kwaya ya Ambassadors of Christ kutoka jijini Kigali nchini Rwanda inatarajia kuwasili saa 9;30 alasiri hii leo katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es salaam wakitokea nchini kwao Rwanda, tayari kwa ajili ya kutoa huduma ya uimbaji katika mkutano mkubwa wa kimataifa unaofanyika katika viwanja vya Biafra Kinondoni jijini Dar es salaam.

Kundi la kwanza la kwaya hiyo liliondoka jana kwa njia ya basi kuja jijini, huku kundi la pili ndio litawasili kwa ndege mchana wa leo.

Hii itakuwa mara ya nne kwa waimbaji hao kufika nchini ambako wamekuwa na mashabiki lukuki, kutokana na uimbaji wao, ambapo safari hii wanatarajia kuwepo kwa wiki nzima jijini Dar es salaam ikiwa maalumu kwa mkutano huo,Pia wanatarajia kuwasili na toleo lao jipya la kanda ambalo baadhi ya nyimbo zimeanza kusikika katika vituo vya radio kama Wapo Radio Fm pamoja na Morning Star radio zote za jijini hapa.



Kanda mpya ya Ambassadors of Christ Rwanda.

Comments