RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

AFRICAN GOSPEL MUSICS AWARDS KUMALIZIKA KWA KISHINDO

Siku ya jumamosi jijini London nchini Uingereza kumefanyika tukio kubwa la utolewaji wa tuzo za Africa Gospel Music Awards(AGMA) 2012, tukio hilo ambalo watanzania wengi walikuwa na matarajio ya kuona mwimbaji wao pekee aliyependekezwa kuwania tuzo hizo katika vipengele viwili kushindwa kupata tuzo hizo kutokana na kura alizopigiwa kuwa chache hivyo kuwapa mwanya waimbaji wengine aliokuwa akiwania tuzo hizo kuondoka na tuzo hizo, bofya hapa kujua washindi.
Onyesho hilo ambalo lilianza kwa kupooza kutokana na watu kuchelewa kuanza kuingia ukumbini pia asilimia kubwa ya watu hata walipoingia ukumbi huo ulio chini ya El shaddai Christian Centre waimbaji waliokuwa wakiimba hawakuweza kuwafanya watu hao wasimame zaidi ya kufurahia huduma yao kwa kuwapigia makofi mara walipomaliza kuimba. Shughuli hiyo ambayo iliongozwa na washereheshaji (MC) wapatao wanne wakiwemo waimbaji kama Diana Hamilton, Rebecca, Wole Awola na mwenzao ambaye ni mchekeshaji aliyeweza kuwavunja mbavu kwa vicheko kutokana na lafudhi na vichekesho hivyo kuwahusu hasa watu kutoka Afrika magharibi ambao walikuwa wameujaza ukumbi huo.
Mwanadada Emmy Kosgei kutoka nchini Kenya ambaye usiku huo alijishindia wimbo bora wa mwaka ndiye aliweza kusimamisha watu waliokuwepo ukumbini hapo kwa jinsi alivyoweza kuimba kwa ustadi nyimbo zake mbili ukiwemo Ololo ambazo kila wimbo aliimba kwanza kwa CD kisha wanamuziki waliokuwepo kuendeleza live mara ulipoisha kwakuwa hawakuweza kufanya mazoezi kabla, mwimbaji huyo aliweza kuwa nyota usiku huo kwani baada ya tamasha nusu ya watu walioujaza ukumbi huo walimzunguka kutaka kupiga picha naye pamoja na kuchukua mawasiliano yake.
Kundi la Makoma ambalo halikuweza kupata tuzo yoyote usiku huo halikuweza kufika ukumbini hapo kwa wakati kutokana na taarifa zilizopatikana baadaye kwamba walipata ajali wakiwa njiani kuja ukumbini hapo ndio maana hawakufika ingawa walituma meneja wao pamoja na mmoja wa waimbaji wa kundi hilo ambaye alipozungumza na GK akasema Makoma wapo vizuri, Mungu akipenda wanapanga kuja Tanzania mwakani.

              ANGALIA BAADHI YA PICHA AMBAZO GK ILIZIKUSANYA SIKU YA TUKIO
                           
Mwanadada Emmy Kosgei kutoka nchini Kenya
.
                           
                           
ANGALIA PICHA ZINGINE, BONYEZA HAPO CHINI
                           
                           
                           
                           
                           
                          
                           
                           

Comments