RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

CHEMSHA BONGO NA BIBLE


Mtunzi wa maswali: Rulea Sanga

LEO NI MARUDIO YA MASWALI TULIYOULIZANA KATIKA CHEMSHA BONGO NA BIBLE YA SEHEMU YA 1-3

Nakuomba usali kabla hujaanza hili zoezi la kujibu maswali ili Mungu aweze kukusaidia kujibu kwa makini, na baada ya kujibu yakusaidie katika maisha yako. Amen

"Jamani hili ni jibu sahihi, mbona mnanibishia. Ngoja tuangalie majibu hapo chini kama sio kwe!!!"

Tunawaomba na nyinyi wadau wa blogu hii muwe na vikundi ikiwezekana ili kufanya discusion kwa pamoja, hii itasaidia sana


SEHEMU YA TATU
CHEMSHA BONGO NA BIBLE- itatusaidie wewe na mimi kuijua Biblia na kumpenda Kristo. Nitakuwa nauliza maswali katika kitabu  fulani, kwa mfano mwezi huu wa Julai tutakuwa tunaulizana maswali katika kitabu cha MATHAYO na mwezi unaofuta itakuwa kutoka katika kitabu kingine.

Mwisho wa mwezi kutakuwa na mtihani ambao utaufanya bila ya kuangalia katika Biblia yako. Ninaamini wewe umeokoka kwahiyo hutaweza kunidanganya kwa kuangalizia katika Biblia.

NB: Naomba usiangalie majibu kabla hujajibu kutoka katika akili yako:

MASWALI KUTOKA KATIKA KITABU CHA MATHAYIKIWA NU MARUDIO YA MASWALI YALIYOPITA

  1. Malaika alipomtokea Yusufu katika ndoto kuwa aondoke na amchukue mtoto na mamaye waende nchi ya Israel. Je, mfalme Herode alikuwa ameshakufa au mzima?

  2. Malizia mafundisho ya Yesu kwa wanafunzi wake

    (i)  Ninyi ni chumvi ya dunia, lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee?..............................................................................................................

    (ii) Ninyi ni nuru ya……………………………………………………

    (iii)  Msidhani ya kuwa nalikuja kuitugua torati au manabii; la,……………………………………………….

    (iv) Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako
    ana neon juu yako --------------------------------------------------------

    (v) Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, ----------------------------------------------------------

    (vi) Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akikupigaye shavu la kuume,-------------------------------

    (v) Wapendeni adui zenu, waombeni wanaowaudhi, ili mpate kuwa wana wa Baba yenu wa mbinguni,---------------------------------------------------------------------------

  3. Taja majaribu aliyojaribiwa Yesu alipokuwa nyikani

  4. Chagua jibu sahihi
    Baada ya Yesu kumgusa mwenye ukoma kwa mkono wake na kutakasika, Yesu akamwambia
    (a)  Angalia nenda ukawambie na wenzako, na kumuonyesha kuhani wako
    (b) Angalia usimwambie mtu, ila enenda zako ukajionyeshe kwa kuhani ukaitoe sadaka kama alivyoamuru Musa iwe ushuhuda wako
    ( c) Angalia nenda na ukamsujudu Mungu wako na kuhani ukaitoe sadaka kama alivyoamuru Musa iwe ushuhuda wako

  5. Jibu NDIYO au HAPANA katika maswali yafuatayo:-

    (i) Je, Yohana Mbatizaji alishawahi kufungwa?

    (ii)Yesu alipokuwa akitembea kando ya bahari ya Galilaya aliona ndugu wawili Simoni na Petro na aliwambia, nifuate nami nitawafanya wavuvi wa watu.

    (iii) Yesu alisema, mkiwasamehe watu  makosa yao Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi, bali msipowasamehe watu makosa yenu, Baba yenu wa mbinguni atawasamehe

    (iv) Yesu anasema tunapofunga tusiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana, kwa maana hujiambia nyuso zao ili wasionekane wamefunga.

    (v) Je, ni kweli Yesu alisema tuyasumbukie ya kesho, kwani hakuna atakayetusumbukia katika suala la kula na kuvaa
MAJIBU
  1. Alikuwa maekufa (Mathayo 2:20)

  2. Mafundisho ya Yesu kwa wanafunzi wake:-

    (i)  Ninyi ni chumvi ya dunia, lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee?, Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu. (Mathayo5:13)

    (ii) Ninyi ni nuru ya ulimwengu (Mathayo5:14)

    (iii)  Msidhani ya kuwa nalikuja kuitugua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza (Mathayo 5:17)

    (iv) Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neon juu yako, iache sadaka yako mbele ya madhabah, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kasha urudi uitoe sadaka yako. (Mathayo 5:23)

    (v) Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, ameshakwisha kuzini naye moyoni mwake (Mathayo 5:27)

    (vi) Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akikupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili (Mathayo 5:39)

    (v) Wapendeni adui zenu, waombeni wanaowaudhi, ili mpate kuwa wana wa Baba yenu wa mbinguni, maana yeye huangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio na haki. (Mathayo 5:43)

  3. Majaribu ya Yesu

    (i) Mawe yawe mikate

    (ii) Yesu kujitupa chini kutoka katika kinara cha hekalu

    (iii) Kumsujudia Ibilisi (Mathayo 4:4:12)

  4. 2.      Baada ya Yesu kumgusa mwenye ukoma kwa mkono wake na kutakasika, Yesu akamwambia, (b) Angalia usimwambie mtu, ila enenda zako ukajionyeshe kwa kuhani ukaitoe sadaka kama alivyoamuru Musa iwe ushuhuda wako (Mathayo 8:4)

  5. Majibu yake ni:

     (i) NDIYO (Mathayo 4:12)

    (ii) HAPANA - Yesu alipokuwa akitembea kando ya bahari ya Galila aliona ndugu wawili Simoni aitwaye Petro na Andrea nduguye na aliwambia, nifuate nami nitawafanya wavuvi wa watu  (Mathayo 4:18-20)

    (iii) HAPANA- Anasema tkiwasamehe Baba yetu atatusamehe na tusipowasamehe na Yeye hatatusame (Mathayo 6:14)

    (iv) HAPANA- Ansema tusiwe kama wanafiki ili tuonekane tumefunga (Mathayo 6:16)

    (v) HAPANA-Yesu anasema tusisumbukie ya kesho, kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe, balo tutafute kwanza ufalme wake, na haki yake na hayo yote utazidishiwa.


Comments