RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

CHEMSHA BONGO NA BIBLE


Mtungaji wa Maswali: Rulea Sanga

CHEMSHA BONGO NA BIBLE 


Inatusaidie wewe na mimi kuijua Biblia na kumpenda Kristo. Nitakuwa nauliza maswali katika kitabu  fulani, kwa mfano mwezi huu wa Julai tutakuwa tunaulizana maswali katika kitabu cha MATHAYO na mwezi unaofuta itakuwa kutoka katika kitabu kingine.

Mwisho wa mwezi kutakuwa na mtihani ambao utaufanya bila ya kuangalia katika Biblia yako. Ninaamini wewe umeokoka kwahiyo hutaweza kunidanganya kwa kuangalizia katika Biblia.

NB: Naomba usiangalie majibu kabla hujajibu kutoka katika akili yako:
SEHEMU YA NANE


MASWALI

1.      Yesu alijibu nini pale alipoulizwa, ni nini dalili ya kuja kwakona ya mwisho ya dunia?

2.      Ni kitu gani Yesu aliwambia wanafunzi wake, baada ya dhiki itakayotokea siku ya mwisho;  kitu gani kitaokea?

3.      Yesu anasema ni nani ajuaye siku ya mwisho?

4.      Kwanini Yesu anatuambia tukeshe?

5.      Kutoka na mfano alioutoa Yesu kuhusia na wale watumwa waliopewa talanta na bwana wao. Wakwanza alipewa talanta taono, wapili akapewa talanta mbili na watatu akapewa talanta moja.

(i) Ni mtumwa yupi alipeleka talanta zaidi baada ya kufanya biashara

(ii) Ni mtumwa yupi alificha talanta na hakurudisha kwa bwana wake.

(iii) Ni kitu gani alimwambia mtumwa wake aliyerudisha talanta zaidi ya zile alizopewa mara ya kwana


MAJIBU
1.      Yesu akajibu akawambia,

(i) Angalieni mtu asiwadanganye, kwa maana wengi watakuja kwa jina langu, wakisema mimi ni kristo; na watadanganya wengi.

(ii) Nanyi mtasikia habari za vita na matetesi mengi ya vita; angalie msitishwe kwa maana haya hayana budi kutukia, lakini ule mwisho bado

(iii) Taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufame kupigana na ufalme

(iv) Kutakuwa na njaa na matetemeko ya nchi mahali mahali

(v)  Wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki, nao watawaua, nanyi mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa yote kwaajili ya jina langu.

(vi) Manabii wengi wa uongo watatokea, na kuwadanganya wengi

(vii) Na kwasababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapotea n.k (Mathayo 24:1-nakuendelea)

2.      Vitu vitakavyotokea baada ya dhiki ni
(i)  Litatiwa giza na mwezi hautatoa mwanga wake na nyota zitaanguka mbinguni

(ii) Nguvu za mbinguni zitatikisika.

(iii) Isaha ya mwana wa Adamu itaonekana mbinguni

(iv) Mataifa yote ya ulimwengu yataoombeleza

(v) Mwana wa Admu ataooneka akija juu ya mawaingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi (Mathayo 24: 29-31)

3.      Yesu asema, walakini habari za siku ile na saa ile hakuna ajuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake. Kwa maana kama ilivyokuwa siku ya Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa, kuja kwake Mwana wa Adamu (Mathayo 24:36:41)

4.      Tukeshe kwa maana, hatujui siku ipi atakuja Bwana wetu (Mathayo 24:42)

5.      (i) Ni yule wa kwanza aliyepewa talanta tano 

(ii) Ni yule wa tatu aliyepewa talanta moja

(ii) alimwambia, “Vema mtumwa mwema na mwaminifu kwa machache, nitakuwekea juu ya mengi, ingia katika furaha ya bwana wako
(majibu yote yanapatikana Mathayo 25:14-21)

Comments