RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

JOHN SHABANI KUTOA VIDEO MPYA. JIPANGE KUIPAT

Mwandishi: Rulea Sanga
Picha na John Shabai
RuMa AfricA inakupongeza John Shabani kwa juhudi zako za kufanya kazi ya Mungu. Ninabarikiwa sana na kazi yako. Umekuwa mfano mkubwa sana kwa waimbaji wa nyimbo za injili Tanzania. Zidi kufanya kazi ya Mungu na usikate tamaa. Tunatambua katika huduma uliyonayo kuna changamoto nyingi kama kuibiwa nyimbo na pengine kudharauliwa na watu wasio mjua Mungu. Kaza kamba na umwangalie Mungu tu na usiangalie ya wanadamu.
Umefika wakati wa kumuunga mkono mtumishi wa Mungu kwa kununua kazi zake alizozifanya na kazi hii mpya mbayo inaenda kutoka karibuni. Hebu kuwa mshabiki wa mambo ya Mungu. Natamani siku moja nikija kwako nione kabati lako la CD / DVD limejaa kazi za Mungu.

Naomba uangalie maandalizi ya kazi yake mpya.

John Shabani na kundi katika maandalizi ya kurekodi mkanda wa video

Albam hiyo mpya iliyoshirikisha waimbaji mbalimbali kama Upendo Kilahiro, Jane Miso, Cosmas Chidumule, Faraja Ntaboba - Kongo, Destiny Sisters - Uganda na wengine kibao, itakamika baada ya miezi kadhaa. Maombi yako yanahitajika sana.






John Shabani na kundu lake la watoto

John Shabani na Upendo Kilahiro

Comments