RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

TAMASHA LA MAOMBI NA UPONYAJI KUFANYIKA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI B ASSEMBLIES OF GOD

Kanisa Mlima wa Moto Mikocheni B Assemblie of God linakukaribisha katika tamasha litakalofanyika katika kanisa hilo. Mchungaji wa kanisal hilo, anakukaribisha sana ili ubarikiwe na uimbaji na Neno la Mungu litakalohubiriwa katika kanisa hilo

Kutakuwa na uimbaji kutkoka kwa waimbaji mbalimbali na bila kusahau waimbaji kutoka kanisa hilo, Happy Kwaya na Joys Bringers watoto wa mama.

Ibada itaanza saa nne asubuhi na kuendelea na kuanzia saa mbili kutakuwa na Sunday School.
Fika mahali pale bila ya kuchelewa ili ujionee ni jinsi gani watu wanamtumikia Mungu kwa njia mbalimbali.

Kwa maelezo zaidi, endelea kusikiliza Praise Power Radio kujua mengi kuhusiana na tamasha hilo litakalokuwa tishio jijini Dar es Salaam.

Mchungaji Getrude Rwakatare pamoja na Crew nzima ya wachungaji wamejipanga vizuri kuhakikisha tamasha linafanyika vizuri na jina la Yesu linainuliwa.


Kanisa liko Mikochen B, panda magari yanayoelekea Mwenge na ukifika Mwenge utaona bajaji nyingi katika njia ya kuelekea katika kiwanda cha Coca Cola. Uliza nataka kufika kwa Mama Rwakatare au Kanisa la Mlima wa Moto. Kama utaona magari ya St Marys ingia yatakufikisham bila ya kulipia chochote

Karibuni Sana

Mwandishi: Rulea Sanga

Comments