RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MASOMO KUTOKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI B ASSEMBLIE OF GOD MWAKA 2008



IBADA YA JUMAPILI KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI B ASSEMBLIES OF GOD  16/10/2008

SUNDAY SCHOOL
MASHUJA-
Mchungaji Kyando

Mchungaji Kyando

Katika kitabu cha Samweli 2:23:8-32, Daud alipakwa mafuta awe mfalme. Alikuwa na kikosi cha kutembea naye.

Tunatakiwa kuwa shujaa wa adui zetu kama vile wachawi, waovu, majini n.k. Tusiwakimbie adui zetu bali kutamba mbele za madui zetu kwamba tunawaangamiza.
Mungu anatafuta shujaa ambaye atavumilia taabu za adui shetani.. Mashujaa wanatakiwa kuteka nyara silaha za adui. Shujaa anatakiwa kuwa na moyo wa kutete watu wake. Na kanisa lake kwa maombi. Mungu anatka shujaa wa mashujaa kwa mfano muombaji wa waombaji, mfariji wa wafariji, mcha Mungu wa wawacha Mungu. Mungu ataka shujaa asiyeogopa kitu chochote ambacho adui shetani anafanya. Mungu anatafuta shujaa wa kupambana na kupigana na shetani au adui.
NB: Samweli 1:17:41-50, kulikuwa na mashujaa 33 na akawachagua mashujaa 3 mma katika hao 3 akamchagua 1. Kuna shujaa alikuwa mwekundu na mzuri ambaye ni Daudi, alipigana na Goliati ambaye ni mrefu sana kiumbo na alivaa gamba la chuma kifuani na alikuwa na nguvu sana.
Nguvu za viata za kupigana nazo ni kama chuki, fitina, uongo, uvivu n.k. Tusome Waamuzi 6:12, 7:20-23, Wafalme 2:24:12-16. Kumbuka ya kuwa adui anajua maana ya mashujaa katika nyumba ya Bwana.

Mungu akubariki
Mchungaji Kyando.

NENO LA UTANGULIZI


UPENDELEO WA MUNGU
-Mchungaji Mlenda
Tusome Methali 14:35, Hesabu 12:1-8)
Upendo wa Mungu uko katika kila kanisa. Upendeleo wa Mungu kwa watumwa wa Mungu. Upendeleo ni sehemu ya upendo. Baraka ni upendeleo wa Mungu kupata vitu vya ziada au baraka ni upendeleo wa neema ya kuwa na vitu. Watu waliokoka ni wapole na sio watu wakubishanana watu, kama mlokole unatakiwa kusamehe watu, kusahau na kupendana tena. Upendeleo wa mfalme ni kwa mtumwa wake atendae kwa akili. Tusiwe washirika wa kawaida bali watofauti. Tusiwe washirika wa kuzoea ibada za kila siku, ila kila ibada unayoingia fanya ni kama siku yako ya kwanza kuhudhuria.

Mungu awabariki
Mchungaji Mlenda

NENO KUU

KUONDOA ROHO YA KUFANYA KAZI KWA UZITO-Mchungaji Getrude Pangalile Rwakatare

Mchungaji Rwakatare

Watanzania mara nyingi ni wataratibu sana. Kuna roho imewafunga kwa kuwafanya watu wa kufanya mambo yao kwa utaratibu sana. Hata ikiangalia maongezi yao na kutembea kwao. Mabadiliko yetu ya kimaendeleo yanaenda taratibu sana kwasababu ya uvivu tulionao. Tumekuwa si wepesi wa kutaka maendeleo kwa kufanya kazi kwa bidii. Tumekuwa na roho  nzito ya kujiendeleza na masomo, na tunaridhika na elimu duni tuliyonayo. Tunatakiwa kuwa na mabadiliko ya kimaendeleo na kuwa na wivu wa kutamani kuwa mabilionea kwa kujibidiisha katika kazi. Soma Samweli 2:1:23, tunatakiwa kuwa wepesi na hodari katika utendaji kazi, hatutakiwi kujihurumia au kuchagua kazi. Roho zetu lazima ziwe wazi na kupenda kufanya kazi. Tunatakiwa kushika au kulinda tulicho nacho tusije tukakipoteza. Nyakati 1:12:8, tunatakiwa kuwa “serious” na kazi ya Mungu, tukifanya kazi ya Mungu kwa bisii naye atatupa hamu ya kufanya kazi zetu kwa bidii na kutuondolea uvivu tulionao wa kutopenda kufanya kazi kwa bidii. Isaya 45:2, Mungu anataka kuona mabadiliko katika maisha yako na yangu, hapendi kuona kila siku uko mahali pamoja. Wengi tunamzuia Mungu kutenda kwasababu hatuko wepesi kutenda na kufanya kazi, na kutii. Hatutakiwi kuridhika na mahali tulipo na tuchukie umaskini.

Mungu awabariki
Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B Assemblies of God
Mchugani Getrude Rwakatare.

Comments