RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MCHUNGAJI RWAKATARE ANAKUKARIBISHA KATIKA IBADA YA JUMAPILI KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHEN B ASSEMBLIES OF GOD


Mwandishi: Rulea Sanga

Mchungaji anakuomba wewe Mtanzania kufika katiKA IBADA YA Jumapili katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B. Ibada itaanza saa 3:00am. Anakualika kufika pamoja na jamaa zako ili kumsifu na kumtukuza Mungu. Mungu anapenda kuona wewe unamtumikia kwa upendo na bila ya kusukumwa na mtu yeyeyote.
Ni mengi utayapata katika nyumba ya Bwana, na hayo utayapata kutoka na imani yako na utayari wa moyo wako. Njoo mpendwa tumtukuze Mungu wetu. Huu ni wakati wako wa kufanya kazi ya Mungu, itafika siku utashindwa hata kunyanyua kijiko au kutoa sauti, utatamani kusoma Neno la Mungu lakini utashindwa.

Mimi kama mchungaji nategemea utafika na hutaniaabisha mtumishi wako. Jinsi ya kufika, panda magari ya Mwenge, na ukifika Mwenga uliza njia ya kwenda katika kiwanda cha Coca Cola, hapo utaona Bajaj nyingi na pia utaona mabasi ya St. Marry's secondary School, yatakuleta kanisani bure.

Jumapili hili kutakuwa na uzinduzi wa albam ya Happy Choir ambao utafanyika hapo kanisani kuanzia saa 9:00. Hakuna kiingilio

Waimbaji katika ibada ni Happy Choir na Joys Bringers

Comments