Glorious Celebration ni kundi la waimbaji wa nyimbo za injili
Tanzania ambalo limeunganisha waimbaji mbalimbali kutoka katika makanisa
mbalimbali nchini Tanzania. Kundi hili limefanikiwa sana katika kufanya
kazi ya Mungu. Mungu amekuwa akiwatumia sana waimbaji hawa katika kazi
yake kwa njia ya uimbaji na katika maombi. Mpaka sasa kundi hili
limefanya kazi ya Mungu katika mikoa mbalimbali ikiwemo Morogoro Dar es
Salaam, Arusha, Dodoma n.k.
Waimbaji hawa
wako chini ya mlezi wao na mbeba maono wa kulianzisha kundi hili, Askofu
Mwakang'ata ambaye anakanisa lake Chang'ombe Dar es Salaam linaloitwa
Full Gospel Victory Church. Mungu amemtumia Askofu huyu kwa kumpa uwezo
wa kununua vifaa vyote vya muziki na kuwalea waimbaji hawa kimwili na
kiroho.
Kipindi cha nyuma kundi hili lilikuwa linatoa
huduma yao ya uimbaji katika hoteli ya The Atriums Siza Afrikasana, na
baada ya muda likaamua kusimama kidogo kutokana na kazi kuwa nyingi za
kufanya kazi ya Bwana, kama vile safari za mikoani kuongezeka, na
maandalizi ya albamu yao mpya pamoja na marudio ya shooting ya albamu
yao ya kwanza ya "Niguse"
Glorious Celebration
imebahatika kufanya kazi ya Bwana ikishirikishwa na waimbaji wakubwa
duniani kama Rebeca Malope. Rebeca Malope ni mwimbaji wa nyimbo za
injili Afrika ya Kusini ambaye Pasaka ya mwaka huu alikuja Tanzania
katika kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji. Tamasha hilo liliandaliwa
na Msama Promotion. Mbali na kushiriki katika tamasha hilo, pia Mungu
aliamua kufanya huduma mbele ya raisi JK Kikwete katika tamasha jinngine
la Pasaka la Msama Promotion.
Glorious Celebration kwa
sasa iko katika maandalizi yao ya kurudia shooting ya albamu yao ya
kwanza ya "Niguse" na katika maandalizi mengine ya albamu yao mpya ya
pili.
Meneja Masoko wa Glorious Celebration, Rulea
Sanga anawashukuru sana wapenzi wa nyimbo za GC kwa kuwa-support katika
kununua CD na DVD zao ambazo ziko sokoni. Rulea aliendelea kuwaomba
wadau wote wa GC kuwa na moyo huo huo katika kazi ya Mungu na kufanya
hivyo hata kwa waimbaji wengine wa nyimbo za injili, kwani kwa kununua
kazi zao, mnawatia moyo sana. Aliwashukuru sana watu wa media kwa kupiga
nyimbo zao katika radio,
Davina (kushoto) na Nice wakisoma Neno
Mercy akiwa amejaa uwepo wa Mungu baada ya kupata Neno kutoka kwa Nice aliyekaa chini akisoma Biblia
Nice alivyokutwa na mpiga picha katika chimbo la kumtafuta Mungu
Nice akiwa na furaha
Davina naye......
Chakula ni muhimu kwa kila mtu, OG kushoto na Lispa wakiaandaa msosi
Mzee wa solo a.k.a Imma Solo akilitekenya gitaa
Mambo mazuri hayaji kwa kujilegeza, fanya kazi na Mungu atakuinua, Emmanuel Mabisa
Choka mbaya, Ima Solo
Nice
Jamani kituguuu machoni
Paul na Neno
Alex Kisonga akikuna nazi
GLORIOUS CELEBRATION WAKIELEKEA PRAISE POWER RADIO KWA MAHOJIANO
Mtangazaji
na meneja wa Praise Power, George Mpela akiwahoji Glorious Celebration
kuhusiana na tamasha lao pale The Atriums Hotel
GLORIOUS CELEBRATION WAJICHIMBIA KAMBINI TENA
Daniel Kibambe akitafuta cha akipambana na dafu, ili apooze koo
Emmanuel Malisa akipambana na bonge la muhogo..yote maisha
Kutoka kushoto ni Angel Benard Lyamba akisoma Neno, David mna Paul wakitafakari Neno
Ombeni Godwin katikati akiwa na wenzake
Duuh....Gospel akiwa amechoka...
Daniel Kibambe akiwa anafikiria jinsi gani ya kumfurahisha kwa njia ya
Usafi muhimu, Chaka
Kazi iansonga, Mungu atafanya tu...
Kama binadamu unaweza kuchoka, Nice Marando akionekana kuchoka
Angel Benard Lyamba....
Dada wa Yesu, Jessica Honore akiwasiliana na jamaa zake, huku akiwa ameshikilia kipande cha bagia
Kama binadamu unaweza kuwa na mawazo fulani, Emmanuel Malisa
GLORIOUS CELEBRATION WAKIFANYA HUDUMA KATIKA UKUMBI WA PRINCE SINZA MORI .
Ombeni Gondwini akitomasa Kinanda taratibu.
Mpiga Drams Baraka Ngoi a.k.a Bwasheee''
Mpiga Bas Emmanuel Materu.
Erick Brighton mtangazaji wa Praise power a.k.a OP.
GLORIOUS CELEBRATION GOSPEL LIVE BAND NDANI YA ARUSHA
Hapa tulikuwa tunatoa huduma katika kongamano la vijana Arusha chini ya kanisa la Bethel Desenba 2011
GLORIOUS CELEBRATION WAKIMTUMIKIA MUNGU NDANI YA THE ATRIUMS HOTEL SINZA SIKU YA IJUMAA 3 Feb 2012
Waimbaji wa Glorious Celebration wakimtumikia Mungu ndani ya The Atriums Hotel
Paul Tonex (aliyenyanyua mkono) akimwimbia Mungu
Mtalaamu
wa Blogs, Website na Graphics Tanzania, Rulea Sanga akiingiza stories
za Glorious Celebration katika hotel ya The Atriums Sinza Afrikasana.
Mtangazaji wa Wapo radio, Silas Mbise kulia akitokelezea na rafiki yake
GLORIOUS WAKIWA NDANI YA KIWANJA CHAO CHA KUMTUMIKIA BWANA-THE ATRIUMS HOTEL, SINZA AFRIKASANA
GLORIOUS CELEBRATION WAKIFANYA KAZI YA BWANA KATIKA KANISA LA CANAAN, UPANGA DAR
GLORIOUS CELEBRATION NDANI YA KANISA LA KKKT MBEZI-DAR
kutoka kulia ni Davina, Mercy, Angel, Ester, Chaka, Imma Malisa
KONGAMANO LA VIJANA KANISA LA KKKT KATIKA SHULE YA SEKONDARI YA FILBERT BAY-KIBAHA
Mwimbaji wa Glorious Celebration, Dany Kibambe akimwimbia Mungu wetu
Waimbaji wa Glorious Celebration
Mkurugenzi wa RUMA, Rulea Sanaga na ni Meneja Masoko wa Glorious Celebration (aliyevaa penzi) akiwa mapumzikoni
Mwimbaji, mpiga kinanda na mpigaji wa drums, Danny Kibambee akiwa katika uwajibikaji
Imma Base kushoto na Ombeni Godwin OG kulia
Nyamaka Tweve akipiga picha
Walioamua kuokoka siku hiyo


Comments