RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BLOGGER WENU RULEA SANGA NIMEFIWA NA BINAMU YANGU NOEL MJINI MBEYA

Ni siku chache nimempoteza mama yangu, na leo nimefiwa tena na binamu yangu mjini Mbeya. Naamini yote ni mipango ya Mungu. Nakumbuka wakati namuaga mama yangu na kumpeleka katika nyumba yake ya milele, nilikutana marehemu binamu yangu na kunipa pole, kumbe alikuwa anamsindikiza shangazi yake ili na yeye baadae amfuate.

Siku anafariki huyu binamu yangu, pia rafiki yake na marehemu mama yangu anayeitwa Mama Hadija Chaula alifariki siku hiyo hiyo mhana. Sijui Mungu alikuwa na mpango gani. Na ninakumbuka wakati niko Mbeya kwenye msiba wa mama yangu, nilienda kumsalimia huyu rafiki na marehemu mama yangu, na alikuwa katika hali mbaya sana, akisumbuliwa figo na maini.

Nawaomba wadau wangu mniombee nifike salama. Mungu awabariki. Nategemea kuondoka leo au kesho.

Comments

Daniel said…
Kaka pole , Mungu akutangulie na awapeni faraja
Safiri salama