RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

CHEMSHA BONGO NA BIBLE

Mtunzi: Rulea Sanga

Kuanzia leo tutakuwa tunaulizana maswali kutoka katika kitabu cha Marko cha Agano Jipya. Ninakuomba ukisome kwa makini ili uweze kujibu maswali yetu vizuri. Juhudi zako za kutaka kujua ya Mungu kutakusababishiwa wewe kuwa karibu na Mungu, na kufanya hivyo Mungu atayaona maisha yako kwa muda wake anaoutaka.

Maswali yanatoka katika kitabu cha Marko 1 mpaka Marko 4

MASWALI

  1. (i) Kwanini watu walimshangaa sana Yesu alipokuwa anafundisha siku ya sabato  katika sinagogi ya Kapernaumu.

    (ii) Ni mtu wa namna gani aliyepasa sauti akisema, “Tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti? Je umekuja kutuangamiza?”

    (iii) Baada ya huyo mtu kusema maneno hayo hapo juu (swali la (ii)), Yesu alisemaje kwa huyo mtu?

  2. Taja miujiza ambayo Yesu aliwahi kuifanya katika kitabu cha Marko.

  3. Malizia misemo ifuatayo aliyosema Yesu:-

    (i) Dhambi zote watasamehewa wanadamu, na kufuru zao watakazokufuru zote, Bali mtu atakayekufuru Roho Mtakatifu…………………………….

    (ii) Kipimo kile mpimacho…………………………………………………

    (iii) Mwenye kitu atapewa na asiye na kitu………………………………..

    (iv) Ni kama punje ya haradani, ambayo ipandwapo katika nchi, ingawa ni ndogo kuliko mbegu zote zilizo katika nchi, ………………………………


MAJIBU
  1. (i) kwasababu alikuwa anafundisha kama mtu mwenye amri wala si kama wandishi.(Marko 1:22)

    (ii) ni mtu mwenye pepo mchafu.(Marko 1:23)

    (iii)  Yesu akamkemea akisema, Fumba kinywa, na umtoke. (Marko 1: 25)

  2. Miujiza

    (i) Alimtakasa mtu mwenye

    (ii) Aliwaponya wenye pepo (Marko 1:32)

    (iii) Alimtakasa mtu mwenye ukoma (Marko 1:40)

    (iv) Alimsamehe dhambi mtu aliyepooza na kumponya (Marko 2:3)

  3. (i) hana msamaha hata milele (Marko 3:28)

    (ii) ndicho mtakachopimiwa, na tena mtazidishiwa (Marko 4:24)

    (iii) hata kile alichonacho atanyang’anywa (Mrko 4:25)

    (iv) lakini ikishakupandwa hukuwa, ikawa kubwa kuliko miti, yote ya mboga, ikifanya matawi makubwa, hata ndege wa angani waweza kukaa chini ya uvuli wake (Marko 4:31)

Comments