RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

ESTER WAHOME NI MWANAMKE PEKEE WA KIAFRIKA ALIYESHIKA NAFASI YA PILI YA MWANANDOA MREMBO DUNIANI.

Ester Wahome kutoka Kenya ni mwanamke mrembo akiwa ni mwanamke mwanandoa wa kiafrika (mweusi) katika shindano la kumsaka mwanamke mrembo wa dunia alioko katika ndoa. Ester aliyeolewa miaka 16 iliyopita alikutana na upinzani mkali kutoka kwa wanandoa wanawake walioko kati ya umri wa miaka 25 na 45 katika shindano hilo lililofanyika mwezi huu.

ESTER WAHOME.

Hata hivyo Ester ambae ni msanii wa muziki wa injiri alikutana na wanawake wazoefu wa mashindano mbali mbali ambao walikwisha nyakuwa tuzo kama za Billboard, huku Ester akidai hajawahi hata kushika top 20 yoyote.

Niwakati muafaka sasa kwa wanawake wa kiafrika kutambua thamani yao, uasili wao heshimana uaminifu  katika  ndoa zao kwani tuzo haziji tuu kwa kuimba au kuigiza filamu, bali kwa yale mazuri wayafanyayo katika jamii. Ukimuangalia  Ester hapo juu, amevaa shingoni mkufu na hereni za asili, kiukweli amependeza.

      ESTER
Pete hii uionayo mkononi, ilizingatiwa na kuheshimiwa, hivyo kuleta matunda kwa mwanandoa mrembo na muimbaji wa muziki wa injiri "Ester Wahome" kutoka Kenya kuipatia heshima Afrika.
 
Source: http://annapita.blogspot.com/

Comments