RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

GOSPEL HOUSE OF TALENT IKIGAWA MAFUNZO KWA WANAFUNZI WAKE IKIWA NI SIKU YA PILI TOKA WAMEANZA

Mwandishi: Rulea Sanga

Ruma Africa inakushukuru James Temu kwa picha zako nzuri ambazo leo zitaenda kuwa baraka kwa wadau wangu wa Ruma Africa, nainakushukuru sana na Mungu azidi kukubariki kwa juhudi zako ambazo unazifanya.

Gospel House of Talent kwa kweli mnafanya kazi ya Mungu kwa upendo wa Agpe, Mungu ninayemwamini mimi Rulea Sanga awabariki na muendelee na kazi ya Mungu. Kazi yenu inataleta matunda makubwa sana katika kizazi hiki na  kizazi kinachokuja. Watu wangapi wana mapesa lakini hawafanyi kazi kama mnayofanya na wamebaki kuwa watoaji tu makanisani na wengine kumaliza katika anasa. Lakini ninyi mmefikiri na kuona ya kuna watu wanaweza kuwezeshwa na wakafanya kazi ya Mungu kwa kupitia vipaji vyao.

Gospel House of Talent chini ya Mchungaji na Mc Haris Kapiga ambaye pia ni Mtangazaji wa Clouds Radio ya jijini Dar es Salaam jana walikuwa katika kazi kubwa na Crew yake kutoa masomo kwa wanafunzi wao ambao wamegawanyika katika makundi mbalimbali kutokana na vipaji au karama zao. Kulikuwa na mafunzo kwa waigizajiwasanii wa muziki, na wana mitindo. Zoezi lilifanyika kwa mafanikio makubwa sana.

Tunaamini baada ya zoezi hili kuisha kutapatikana watu wakali na wenye usongo wa kumtangaza Kristo kwa njia ya sanaa, na hii itakuwa changamoto kwa wachungaji na waimbaji ambao wako katika game kwa muda mrefu sana.

Huu ni wakati wako kama mwanadamu na mwenye akili zako timamu kufanya kazi ya Mungu kwa kupitia karama yako,  kwani ipo siku hutapata hata dakika ya kuongea na rafiki yako pale utakapobanwa na kuwa kitandani ukishindwa hata kutamka neno lolote. Siku za kuisha hapa dunia zinahesabika na wakati wetu wa kuishi umekwisha sasa. Fanyeni kazi ya Mungu na msiwe watu wa kukaa makanisani tu na kusubiri baraka kutoka kwa wachungaji wenu. Tokeni huko na kwenda kutafuta kondoo waliopotea, na mkishawapata leteni kanisanai na kuwaachia wachungaji wenu wazidi kuwalea nao wakishakomaa watatoka na kwenda porini kutafuta kondoo wenzao waliopotea.

Mchungaji Haris Kapiga alikuwa ni muumni wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B Assemblies of God na alikuwa ni Mtangazaji wa Praise Power Radio ya kanisa hilo, lakini leo ametoka hapo kanisani na kuwachia wengine watangaze, na amekimbilia porini kutafuta kondoo waliopotea. Hivi sasa Mchungaji Haris Kapiga anakanisa lake Kamanyola na amefikiria kutafuta kondoo kwa kuanzisha hii project ya Gospel House of Talent. Mbali na hapo baada ya kutoka katika radio ya Praise Power akaamua kwenda katika radio ambayo sio ya Kikristo na kufanya kazi hapo kwa lengo la kuwaleta watu kwa Kristo. Na Mungu alivyo wa ajabu amempa kipindi cha kulitangaza Neno la Mungu kwa njia ya waimbaji wa nyimbo za Injili.

Ruma Afrika inakupongeza sana Harisi Kapiga kwa juhudi zako, na umekuwa chachu katika kampuni yangu ya Ruma Africa na mimi niko nyuma yako kutafuta kondoo waliopotea kwa kutumia karama yangu hii ya blogging, web deign, Graphics na Movie editing. Ipo siku nitatambulika katika jamii.

UFUNGUZI WA DARASA

Hudson Kamoga: "Bwana Yesu asifiwe"
Wanafunzi: "Ameni mtumishi wa Mungu"

WANAFUNZI WAKIWA DARASANI

Leo watanijua kuwa mimi nani katika kazi ya Mungu!!
Wacha mimi nicheke kwasababu niko na Yesu na leo Mungu amenikumbuka kwa kupia GHT
  Fredy: Unaona kipaji changu? na bado, mtanijua mimi nani..!!

VIONGOZI WA GHT
 Mr. Robert Mng'anya Mhazini wa Gospel House Of Talent  na Harris Kapiga  CEO wa Gospel House Of Talent (GHT)

DARASA LIMEANZA, KILA MTU NA KALAMU YAKE KUCHUKUA NOTES

MWALIMU AKIWA NA WANAFUNZI
Mwalimu: Hudson kamoga: Mtu akifanya vibaya namchapa viboko, sawa?


  Mtangazaji wa Praise Power, James Temu (kushoto) akiwa na rafiki yake Eunice

VIONGOZI WAKIPONGEZANA KWA KAZI YA MUNGU
Haris Kapiga kulia na Hudson Kamoga: Hahahah kazi ya Bwana inalipa, unaonaje Hudson?
Yaaani wewe usisema Haris, inalipa mpaka chenji, cha msingi ni kuwa mnyenyekevu na kufanya yale Mungu anataka.
Angalia Baraka kutoka kwa Mungu zinavyomwagika kama mvua...wewe acha tu!!
Aha hah hah hah. Ooooh Mungu ni mtamu, sitamwacha kamwe !!!!
Hebu lete mkono tumshukuru huyu Mungu kwa kuliwezesha hili zoezi.
Dhu..walimu wetu wamefuahi eh!!
Na sisis ipo siku tutafurahi kama wao ngoja tutoke katika mjengo huu baada ya kuonyesha vipaji vyetu.

KAZI IKIENDELEA KWA UNYESHAJI WA VIPAJI
Sasa ni chezeje Mwalimu?
Imetoka hiyo ikirudi pancha, vijana wangu wako fit, in the name of Jesus !!!
Jamani hata kucheza mnaangalizia...wewe fanya yako na sisi tunafanya yetu.
Kwa raha zangu namtumikia Mungu wangu, na wewe mtumikie Mungu wako

WAKATI WA MAIGIZO
Ulikitaka picha zaidi bonyeza hapo chini palipoandikwa "Read More"


Maigizo hapa ni nyumbani



MA KOMPYUTA TIME
Eunice na Hardson Kamoga: "Unaona picha zilivyo bomba..Temu ni balaa!!

CEO WA GOSPEL HOUSE OF TALENT
 Harris Kapiga:"Jamani mmefuarahia somo?"

Nawshukuruni sana kwa kuja kwenu

WIMBO WA TENZI ZA ROHONI UKIIMBWA
"Naona uwepo wa Mungu, jamani!!"
"Tujipigie Makofi kwa uimbaji"

Comments