RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

RUMA AFRICA: HONGERA SANA DADA JESSICA HONORE KWA SHOOTING:


Mwandishi: Rulea Sanga

Uongozi wa Ruma Africa unakupongeza kwa hatua uliyofikia.
 Jessica Honore ni mwimbaji wa nyimbo za injili Tanzaniani. Kuna kipindi ameimba na kikundi cha Glorious Celebration katika album yao mpya ya "Niguse".

Kama hujawahi kumuona Jessica anaimba naomba uangali hii video yake na utaamini kuwa Mungu anawatu wake wanaweza kumsifa kwa roho na kweli.
Baadhi ya waliotokelezea katiak video hii ni  Boniface Magupa (Mtangazaji wa Channel Ten), kaka yake (mwimbaji wa nyimbo za injili) na wengine wengi kama utakavyowaona katika picha hapo chini.

Jessica Honore ni mtalaamu wa kufanya  Jingles (matangazo redioni) , na alishafanya jingles nyingi katika kituo cha radio cha Clouds FM. Ni mjasiliamali na mtumishi wa Mungu.

Watanzania na dunia nzima naomba mnunue kazi yake itakapotoka ili kazi ya Mungu isonge na wewe upate kubarikiwa na ujumbe kutoka kwa dada yako au mdogo wako Jessica Honore.
Nyimbo inaitwa NAPOKEA
Muimbaji ni JESSICA HONORE
Imefanywa na kampuni ya EXCLUSIVE MEDIA
Director wa video ni GODIE
Video inategemewa kutoka katikati ya wiki ijayo hivyo watanzania wajiandae kupata video bora na ya kipekee, kwani Exclusive Media imekusudia kuleta mabadiliko katika video za mziki wa njili kwa kufanya video zenye ubunifu na ubora wa hali ya juu.

  Director


Walioshiriki





Comments