RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

LOVE TANZANIA FESTIVAL YATIKISA KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM

Ruma Africa ilibahatika kukanyaga katika viwanja vya jangwani kushuhudia matendo makuu ya Mungu. Kwa kweli mimi binafsi niliguswa sana na huduma iliyokuwa inaendelea mahali pale, kuanzia mahubiri, uimbaji, michezao ya baiskeli, michezo ya pikipiki na watu jinsi gani walivyofurika na kuonyesha hali ya kuridhika na kile kilichoandaliwa na Love Tanzania Festival.

Watanzania walionekana kuonyesha moyo wa uzalendo kwa mahudhurio yao, sikutegemea kuona watu wengi kiasi hicho. Nimeamini kuwa sasa muamuko wa kupenda kazi za Mungu umeaanza kuingia nchini kwetu.

Katika Love Tanzania Festival kulikuwa na mambo mengi yakiendelea mahali pale, na baadhi yake ni michezo ya pikipiki na baiskeli, uimbaji kutoka kwa waimbaji wa Tanzania na nje ya nchi, ushuhuda kutoka kwa Mchungaji mtarajiwa Masanja Makandamizaji, Neno la Mungu kutoka kwa wachungaji mbalimbali.

Nimeamini kuwa Mungu amempa kila mtu kipaji ambacho ni cha kipekee na kipaji hicho mwingine amenyimwa. Wewe uliyepewa kipaji fualani jaribu kukitumia kwaajili ya kumtumkuza Mungu. Jana watu walitumia vipaji vyao kama kuendesha pikipiki na baiskeli kwa kiwango cha juu sana na hii ilifanya watu kupiga kelele za furaha kutokana na mbwembwe walizokuwa wanaonyesha kwa kuruka juu sana huku wakichezea vyombo hivyo hewani. Na waimbaji walioiimba kwa kiwango cha juu sana mpaka blogger wenu nikatamani na mimi siku moja kuimba.

MICHEZO YA PIKIPIKI


 

MCHEZO WA BAISKELI


WIMBAJI WA TANZANIA
Pastor Safari akilonga na waimbaji wa kapela The Voice kabla ya kuvamia jukwaa


PRAISE TEAM YA PASTOR SAFARI
Pastor Safari akiimbisha
Upendo Kilahiro akimtukuza Mungu kwa uimbaji
 Pastor Safari.
Sam Yona kushoto na wenzake
Christina Shusho

WATU WALIOHUDHURIA


MCHEKESHAJI NA MCHUNGAJI MTARAJIWA MASANJA MKANDAMIZAJI WA ZE COMMEDY TBC 1
Kuna ushuhuda aliutoa Masanja, ila ulionigusa ni pale aliposema yeye unavyomuonaga anatembea katika luniga kama miguu yake ina mafunza, ni kweli kwani akiwa Kijijini kwake aliliwa sana mafunza na kumsababishia ulemavu wa kutembea hivo. Ila unapomuona anatembea kawaida huo sio mwendo wake, ila huwa anaigiza. Alisema "Anamshukuru sana Mungu kwa kumuokoa na leo hii mnamuona katika majukwaa na wazungu" alimshukuru sana mchungaji wake Mwakiborwa wa Mito ya Baraka kwa kuleta kwa Yesu. Baada ya shuhuda zake nyingi aliimba wimbo wa "Ni Pepo Lishindwe "  ambao ulikonga nyoyo za watu.


Upendo Benson akinyoosha mkono juu kukubali kazi ya Masanja mkandamizaji.
Kushoto ni Masanja Mkandamizaji,Silas mbise na Lyanga George.

DAVE LUBBENI KUTOKA ULAYA


DON MOEN


NICOLE MULLEN
Kutoka kulia ni mtoto wa Upendo Kilahiro, Upendo Kilahiro, Nicole Mullen, Christina Shusho
  
Haya ndio yaliyojiri siku ya jana kupitia viwanja vya Jangwani,Tukutane baadae hapa hapa katika kukupa habari yakile kitakachojiri leo.Barikiwa
MASHABIKI WA YESU




Comments