RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MALKIA WA MUZIKI WA INJILI BAHATI BUKUKU WA "DUNIA HAINA HURUMA" KUUNGURUMISHA JUMAPILI HII KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI B ASSEMBLIES OF GOD

Mwandishi: Rulea Sanga

Bahati Bukuku amekuwa kivutio kwa walio wengi Tanzania kwa nyimbo zake zenye kugusa maisha ya watu. Na sasa Mungu amemtumia sana katika uimbaji wake kwa kumpa wimbo mwingine ambao ni gumzo kwa walio wengi waliousikia, wimbo unaitwa "Dunia Haina Huruma"

Jumapili kama tatu au mbili zilizopita Bahati Bukuku alikuwa katika kanisa la Mlima wa Moto la Mchungaji Kiongozi Getrude Rwakatare akifanya huduma yake, watu walibarikiwa sana, kama utakapoona katika picha.

Jumapili hii atakuwepo kanisani hapo (MLIMA WA MOTO MIKOCHENI B ASSEMBLIES OF GOD), kama hukubahatika kumuoona na kushirikiana naye kupokea baraka kwa njia ya uimbaji, unakaribishwa sana jumapili hii ili kumfanyia sifa Mungu. Kumbuka Mungu kati ya vitu anapenda ni kutukuzwa na kusifiwa kwa njia mbalimbali ikiwepo njia ya uimbaji.

Ibada itaanza saa 3:00 asubuhi. Kutakuwa na waimbaji wengine kutoka katika kanisa hilo ambao ni Happy Kwaya na Joys Bringers. Hwa waimbaji Mungu amewapa karama ya pekee kwa utunzi wao mzuri wa nyimbo. Nyimbo zao zimekuwa zikiwagusa walio wengi na kubarikiwa.

Kama ni mara yako ya kwanza kufika katika kanisa hili, panda gari la kwenda Mwenge, ukifika hapo utaona kuna bajaji nyingi katika eneo la mataa ya trafic, uliza kanisa la mama Rwakatare au utakutana na mabasi ya St. Mary's ambayo yatakupeleka kanisa bila ya nauli.

Angalia picha hizi pale bahati Bukuku alipokuwa Mlima wa Moto

Bahati Bukuku akiimba wimbo wake wa Dunia haina huruma katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B assemblies of God.




Angali mtumishi sura yake, akimaanisha na kile anachokiimba

Mchungaji Kiongozi wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B Aseemblies of God, Mch. Mh. Getrude Rwakatare akikukaribisha jumapili hii kanisani kwake.
Mchungaji Rwakatare akimwangalia Bahati Bukuku akiimba

Waumini wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B Aseemblies of God

Mzeee wa kanisa, Mzee Mziwanda kushoto na mchungaji kutoka Kenya, Francis Junior

Comments