RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

CHEMSHA BONGO NA BIBLE


Mtunzi: Rulea Sanga

ONYO: Jibu swali kwanza kabla hujaangalia jibu lake.
HABARI NJEMA: Kesho kutakuwa na mtihani wa mwisho wa mwezi wa kitabu cha MARKO.
Ruma Africa inaomba ujiandae ili uwe mshindi, na Mungu akupe nguvu na muda wa kusoma kitabu cha Marko.
MASWALI
  1. (i) Vazi alilovaa Yesu ulipokaribia wakati wa  kusulubiwa kwake lilikuwa la rangi gani?

    (ii)  Taja baadhi ya adhabu alizozipata Bwana Yesu kutoka kwa Wayahudi wakati ulipokaribia kusulubiwa?

    (iii) Ni nani alishurutishwa ili achukue msalaba wake?

  2. (i) Nini maana ya Golgotha?

    (ii) Mvinyo aliopewa Yesu ulitiwa nini?

  3. Yesu alisulubiwa saa ngapi pale mavazi yake yalivyopigiwa kura?

  4. Anwani ya mashitaka iliandikwaje juu ya msalaba?

  5. Wanyang’anyi wangapi walisulubishwa na Yesu?

  6. (i) Watu waliokuwa wakipita njiani na kumuona Yesu  amesulubiwa, walisema maneno gani?

    (ii) Wakuu wa makuhani nao walisema nini juu ya Yesu alipokuwa amesulubiwa?

  7. (i) Wakati Yesu amesulubishwa, ilipofika saa sita, kulitokea nini?

    (ii) Ilipofika saa tisa, Yesu alipaza sauti gani?

    (iii) Watu waliosimama mahali pale ambapo Yesu akipaza sauti walisema nini na kile Yesu alikisema?

  8. Ni akina nani walionunua manukato ili wapate kwenda kumpaka Yesu siku ya sabato baada ya Yesu kushushwa msalabani na kuviringishwa jiwe mbele ya mlango wa kaburi?

  9. (i) Mariamu Magadalene, Mariamu mamaye Yakobo, na Salome walipoingia ndani ya kaburi la Yesu ili wampake manukato waliona nini?

    (ii) Ni maneno gani huyo kijan aliyekuwa kaburini aliwambia, Mariamu Magadalene, na Mariamu mamaye Yakobo, na Salome walipoingia kaburini mwa Yesu ili wampake manukato Yesu?



MAJIBU

1.      (i) Rangi ya zambarau (Marko 15:16)

(ii) Wayahudu walimfanyia Yesu yafuatayo:-

            (a) walimvika vazi la zambarau.

            (b) wakasokota taji la miiba, wakamtia kichwani.

            (c) Wakamsalimu “Salamu mfalme wa Wayahudi”

            (d) Wakampiga mwanzi kichwani
           
            (e) Wakamtemea mate

            (f)  Baada ya kuddhihakiwa walimvua lile vazi la zambarau, wakamvika
                  mavazi yake mwenyewe.

           (g) Wakamchukua nje ili wamsulubishe.

(iii) Simoni ndiye alishurutishwa wakati akitoka shambani ili abebe msalaba wake (Marko 15:21)

2.      (i) Golgotha maana yake Fuvu la kichwa (Marko 15:22)

(ii) Walimpa mvinyo iliyotiwa manemane, na hakuipokea (Marko 15:23)

3.      Ilikuwa saa tatu (Marko 15:25)

4.      Iliandkwa MFALME WA WA WAYAHUDI (Marko 15:26)

5.      Walikuwa wanyang’anyi wawili, mmoja mkono wake wa kuume na mmoja mkono wake wa kushoto. (Marko 15:27)

6.      (i) Nao waliokuwa wakipita njiani wakamtukana, wakatikisatikisa vichwa, wakisema, Ahaa! Wewe mwenyekuvunja hekalu na kulijenga siku tatu, jiponye nafsi yako, ushuke msalabani. (Marko 15:30)

(ii) Wakuu wa makuhani wakadhihaki wao kwa wao, pamoja na waandishi, wakisema, hawezi kujiponya mwenyewe. Kristo, mfalme wa Israel, na ashuke sasa msalabani tupate kuona na kuamini. (Marko 15:31-32)

7.      (i) Ilipokuwa saa sita, palikuwa na giza juu ya nchi yot. Marko 15:33)

(ii) Yesu alipaza sauti yake kwa nguvu, Eloi, Eloi lama sabakithani? Maana yake Mungu wangu mbona umeniacha? (Marko 15:34)

(iii) Walisema, Tazama anamwita Eliya. (Marko 15:35-37)

8.      Mariamu Magadalene, na Mariamu mamaye Yakobo, na Salome. (Marko 15:1)

(i) Waliona kijana ameketi upande wa kuume, amevaa vazi jeupe, wakastajabu. (Marko 16:5)

(ii) Aliwambiwa, Msistaajabu, mnatafuta Yesu Mnazareti, aliyesulubiwa amefufuka, hayupo hapa, patazamenimahli walipomuweka. (Marko 16:6)

Comments