RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

VIONGOZI WA DINI CHANZO CHA MIGOGORO--JAJI MKUU MSTAAFU


Jaji mkuu mstaafu wa Tanzania akizungumza.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Augustino Ramadhani, amewataka viongozi wa dini kuacha kuwa chanzo cha migogoro makanisani na badala yake kurudi zaidi kwa Bwana Yesu ili kuweza kutimiliza kusudi walilopewa katika utumishi wao.
Rai hiyo aliitoa juzi siku ya Jumapili katika sherehe za uzinduzi wa miaka hamsini ya Umoja wa Kujisomea Biblia (Scripture Union) zilizofanyika katika ofisi za makao makuu ya shirika hilo maeneo ya Muhimbili wakati alipohudhulia kama mgeni rasmi wa tukio hilo.
Alisema tatizo kubwa lilipo makanisani kwa hivi sasa linasababishwa na viongozi wenyewe ambao badala ya kumtumikia Mungu wamegeuka na kuangalia vyeo hivyo basi ni vyema kurudi kwa Bwana ili waweze kumtumikia.
Migogoro mingi iliyopo makanisani hivi sasa matatizo makubwa yako kwenye uongozi wala sio wanaoongozwa cha muhimu tu ni kwamba viongozi warudi zaidi kwa Bwana wanayemtumikia” alisema Jaji Augustino Ramadhani.
Sherehe hizo zilihudhuliwa na watu mbalimbali wakiwemo Jaji Angera Kileo, Askofu Philemon Tibanenason, Mweka Hazina wa Chuo Kikuu cha Mlimani, Donata Mugassa pamoja na viongozi wa shirika hilo, Mwenyekiti Dk. Edda Mwandi aliyekuwa mwenyeji wa sherehe hizo pamoja na Katibu Rev. Emaus Bandikile.
source--gospelvisiontz.blog

Comments