RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MY DREAMS COMES TRUE BECAUSE OF T.B. JOSHUA: MUUMNI WA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI B ASEEMBLIES OF GOD,RULEA SANGA AOTA NDOTO AMBAYO YALETA MATUNDA TANZANIA

Tarehe 24 Julai 2012 niliota ndoto usiku ambapo kanisani kwangu wagonjwa waliletwa wengi sana wakiongea lugha ya mkoani kwangu Iringa ya Kihehe, wakitukanana kwa kusema, "Kwa ujinga wako wamechomwa moto", walikuwa wanalalamika sana huku wakigeukageuka mpaka nguo zao zinatoka na wanakuwa tupu hawana nguo.

hayo yote yalikuwa yanatokea katika kituo cha radio, Praise Power, nikiwa hapo nilikuwa na mtangazaji wa Praise Power, Victor Haron. Hofu ilizidi kututawala mimi Victor Haron kuwasogelea wale wagonjwa, lakini mimi nikawa na nguvu ya kuwaombea. Niliwasogelea wale wagonjwa na kuanza kuwaombea na wenzangu wakaanza kuwaombea. Nilipoangalia nje nikaona watu wengi sana.

Nikiwa katika hali ya maombi, nikaona Nabii T.B. Joshua wa sinagogi ya SCOAN Lagos Nigeria anaingia, nilikimbia kwenda kumfubgulia mlango, naye akaingia ndani. Baada ya kuingia Nabii T.B. joshua nilifunga mlango ili watu wengine wasiingie ndani ya pale tulipokuwa tunawaombea wagonjwa. Cha kushangaa watu hawakuonyesha moyo wa kuingia wakawa wamekaa nje wanatuangalia

Nabii T.B. Joshua alipoaanza kuwaombea wagonjwa, nikapatwa na nguvu za ajabu za kuombea wagonjwa na kukemea mapepo. Nikiwa nakemea nikawawaa natamka kama vile T.B. joshua na Wise Men wake wanavyokuwa wanakemea kwa kuseme, "Out by the name of Jesus...Out Out Out" kwa hasira.

Baada ya muda Nabii T.B. Joshua aliondoka na kwenda kuwatuliza watu wasipige makelele. TB Joshua akapenda mimi nijitambulishe mbele za watu ni wapi mimi na TB Joshua tumewahi kukutana, nikawaeleza na kusema, "Nimekutana na TB Joshua kanisani kwake Nigeria Lagos, ambapo niliitwa kwenda kumuona kutokana na yeye TB Joshua kupenda blogu yangu", nilipokuwa nataka kuanza kuelezea kuhusiana na blogu yangu, TB Joshua alinikatisha kwasema "Enough" ("Inatosha") nisiendelee kuelezea hilo, nilinyamaza.

Nilipomaliza kujitambulisha nikapata nguvu za ajabu kwa kuwaombea wagonjwa na kukemea mapepo ukilinganisha na mara ya kwanza. Nikiwa naomba kila ninayemgusa huku nikisema maneno kama ya Nabii TB Joshua, "Be healed in the Name of Jesus" ("Upone katika Jina la Yesu"). wagonjwa wakawa wanakataa kuguswa kutokana na vidonda vyao walivyokuwa navyo katika miili yao ambavyo vilisambaa mwili mzima kuwasababisha maumivu makalia.

Mkono mwangu nilikuwanivevaa vitambaa vyeupe vya hospitalini. Niliendelea kukemea kwa kutumia neno la "Be healed in the name of Jesus".

Nilipomaliza kuomba nikaona waislam wako mahali pale tulipokuwa tunaombea wangonjwa (kanisani katika kituo cha Praise Power), wakiwa wamevaa nguo zao ndefu kama gauni za rangi ya khaki inayoelekea katika weusi na kofia zao nyeupe, nao wakiomba huku mikono yao wakiinyosha mbele. Nilipowaona nilishtuka sana, lakini akili yangu akaja na kuona wanachokifanya (kuombea wagonjwa) ni kitu cha kawaida na sio cha kushangazwa. Nilipita katikati yao na kuelekea upande wa Nabii TB Joshua.

Nilipofika kwa Nabii T.B. joshua akawa haendeleei tena na maombezi kwani alikuwa ameshamaliza, na kilichobakia alikuwa anajiandaa kwenda kwa Mchungaji Getrude Rwakatare ili amuage na kurudi kwao Nigeria. Penmbeni ya Nabii T.B. Joshua nikaona akina dada warembo sana wameongozana na Nabii T.B. Joshua, na waliponiona wakaanza kutabasamu tuna hawaongei chochote.

Nabii TB Joshua aliondoka nakuelekea katika mlango wa ofisi ya Mchungaji Getrude Rwakatare, na alipofika hapo mlango ulikuwa umefungwa akafungua kidogo ili kuangalia ndani kuna nani.  Ilionyesha kuwa ndani mchungaji alikuwa na mtu mwingine anaongea naye, na isingekuwa rahisi ya Nabii T.B.Joshua kuingia mpaka huyo mgeni atoke kwanza. Nabii TB Joshua aliegemea mlango kama ishara ya kumsubiria huku kichwa chake kinaangalia juu.

Nilipomuona TB Joshua amesimama peke yake, nikasukumwa na nguvu fulani na kwenda kwake, na nilipofika nilimkaribisha nyumbani kwangu, na yeye alinishika kidevu changu huku akitabasamu na kuchezea kidevu changu kwa muda kidogo, na akasema "I shall come, dont worry" ("Nitakuja, usiwe na wasiwasi"). Ongea yake ilionyesha kuniridhisha na sio kweli atakuja nyummbani kwangu. Na baada ya hapo niliamka usingizini.

MATIKEO YA NDOTO YANGU.


Namshukuru Mungu kwa kupitia ndoto nimeona yafuatayo"

KWANZA//  Tarehe 26. 08. 2012, wainjilisti kutoka katika Sinagogi ya Nabii T.B. Joshua walikuja Tanzania kwa lengo la kuongea na Partners wa Emmanuel TV na kuandikisha wale waliokuwa wanauhitaji wa kwenda Nigeria kwa TB Joshua kuombewa ili wapone na magonjwa yao. Walipofika nilibahatika kuonana nao LIVE na nikaongea na mmoja wa Wainjilisti. Walinipa kazi ya kupiga picha ili niziweke katika blogu yangu.

Na mwaka huu mwezi wa nne nilibahatika kwenda SCOAN baada ya Nabii TB Joshua kunialika kutokana na kazi ya Blogu.

PILI// Mwezi wa saba kuna dada mmoja alikuwa anaumwa sana na anasumbuliwa na mapepo yaliyosababisha kuchukiwa na ndugu zake. Alikuwani mtu wa kutofanikiwa, kila akifanya jambo hafanikiwi. Huyo dada aliingia katika google na kutafuta habari za mtu yeyote aliyewahi kwenda Nigeria kwa Nabii TB Joshua. Na hii alifanya ili aweze kupata Anointing Water. Alipoandika "TB Joshua in Tanzania" akabahatika kukutana na blogu yangu, na akachukua namba yangu ya simu na kunipigia. Nilimuomba tukutane Fast Food, Kwa Remmy Sinza Dar. Tulipokutana alinisimulia mengi sana kuhusiana na chanzo cha mapepo yake.  Nilimpa "Anointing Water" na tukapanga kuonana siku ya pili. Na yeye alienda kuyatumia yale maji nyumbani kwake. Muujiza wa kwanza aliupata ni kwamba katika TV yao, Channel ya Emmanuel TV huonyesha chenga ila baada ya kutumia maji alianza kuonyesha vizuri. Alikuwa anakatazwa na mama yake kuiangalia, lakini akashangaa kuona mama yake ameanza kuiangalia.

Akiwa anasoma aliwahi kuwa na rafiki yake wa kike, huyo rafiki yake alimuomba amchanje bega lake kwa wembe alama ya msalaba, na alipomchanja damu zilitoka nyingi sana. Huyo dada aliyechanjwa amkamwambia "Kuanzia sasa naenda kufanikiwa na wewe utakuwa mke wangu". Dada huyo aliyechanjwa hakuonekana tena hapo shule na hajajulikana ni wapi alienda. Wakati yuko shuleni huyo dada aliyechanjwa hajawahi kuonekana anaoga na marafiki zake bafuni wale kuvua soksi za viatu vyake. Kumbuka hawa walikuwa wanasoma shule ya bweni.

Dada aliyemchanja kuanzia hapo mikosi ikawa inamuandama sana, ndugu zake walimchukia kabisa,hata mama yake mzazi alimchukia. Wifi yake ambaye alimfanyia connection kwa kaka yake amuoe naye alimchukia mno. Alisema, inafika point wanatukana na mama yake.

Shuleni akawa anafeli masomo. Baada ya kumaliza masomo yake ya sekondari alipelekwa India na alipofika huko mambo yakawa magumu sana, hapati usingizi usiku na ni mtu wa mawazo sana, akifanya kazi pesa zinapotea na hajui zimeenda wapi au utaona tatizo linatokea na kufanya kutumia pesa zile anazozipata, akifanya mitihani ya kawaida anafaulu lakini akifanya mtihani wa mwisho anafeli. Yalipotoka matokeo ya mtihani wake wa mwisho huko India, cha kushangaza akaona jina lake halipo, na inaonyesha kama vile hakufanya mtihani. Alirudi Tanzania na kuanza maisha mengine huku akiishi na mama yake. Ndani ya nyumba yao hakuna amani.

Alipobahatika kunipata mimi (Rulea) katika mitandao tulipanga kwenda katiaka kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B kuomba. nilipofika hapo niliongea namtumishi wa Mungu mmoja na kuanza maombi. Maombi yalichukua muda mrefu sana. Yule dada akaanza kutapika sana huku akionyesha kidole chake cha pete. Tuliomba muda wa masaa kama manne none stop. Baada ya muda akatokea Mtumishi wa Mungu Stanley akaomba tumtoe eleni zake za dhahabu, dada akiwa katika hali ya kupagawa na mapepo akawa anakataa kutoa. Tulifanikiwa kumtoa na kuanza maombezi. Tulipomuona akili yake imerudi tuliiita jina lake na yeye hakuweza kuongea, aliomba kalamu ili andike kile kinachomsumbua, naye aliandika kuwa "Sauti haitoki" Tukaanza tena maombi ya kufungua kinywa chake. Mungu akatusaidia,yule dada akaongea.

Baada ya kumuuliza kwanini alikuwa hataki kuondoa heleni, alisema, kuna heleni alipewa na yule dada aliyemchanja, na hajawahi kuiondoa na amekuwa akiipenda sana. Na kuna cheni ya shingoni ambayo nayo alikuwa anaipenda sana, na kila kijaribu kuuza haiuzika, na mtu akitaka kununua atataka kuuziwa kwa bei ya chini sana.

Tuligundua kuwa yule dada alifungwa ndoa na hilo jini. kwani kuna muda alikuwa akionyesha kidole chake cha ndoa.

Mpaka sasa naongea, huyu dada amani ndani ya familia yake imerudi na sasa yuko India kufanya mtihani wake aliofeli.

Hitimisho ni kwamba ndoto yangu ya kuombea wagonjwa na kupona ilitima

ASANTE MUNGU


Comments

Unknown said…
asante kwa shuhuda nzuri mimi pia ni mtazamaji mzuri wa emmanuel tv nahitaji annointing water