RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

RULEA SANGA KUJIFUNZA NENO LA MUNGU KUHUSU SAFARI YETU YA MBINGUNI NA HABARI NJEMA KATIKA KANISA LA EFATHA MWENGE JUMAPILI YA JANA.


Mwandishi: Rulea sanga
Ombi: Tusamehane kama kuna makosa ya Kiswahili


Mungu aliniwezesha kufika katika kanisa la Efatha Mwenge jijini Dar es Salaam, linaloongozwa na Nabii Josephate Mwingira. Ibada ilikuwa na uppako wa kipekee, binafsi niliguswa sana na Habari Njema nilizopata kwa mhubiri wa Jumapili hii, mke wa Nabii Josephate Mwingira anayeitwa Lyapunda. Naye alianza kwa kusema:
Ninazo Habari Njema kwako. Injili ni Habari Njema iletayo Wokovu, inawezekana masikioni mwako ikawa sio nzuri, lakini ni Habari Njema.za kubadilisha maisha yako kama utazipokea na kuzikubali ndani ya moyo wako.

Tutafute kwanza Ufalme wa Mungu na hayo mengine ni nyongeza ambazo tutaziacha hapa duniani lakini Habaru Njema ni za milele. Tusome Wakoritho 1:5:7, Yesu alikufa msalabani kutuookoa, ila ametupa maagizo ya jinsi ya kuishi kama watu tuliokoka. Tusiishi kama chachu ya kale ya uovu na tabia zote za kale na kuanza maisha mapya. Mwenendo au tabia yako ya kale inatakiwa kubadilika. Tujitakase na kujisafisha kuwa donge jipya la pasaka ambaye ni Yesu aliyetolewa kwaajili yetu.

Tuwe weupe wa moyo na kuona kweli  iko ndani yetu. Tusichangamane na wazinzi, wanyang’anyi, waongo, wenye dhambi, lakini tusiache kabisa kwasababu wote tuko duniani. Tulioko kanisani tusichangamane na hao watenda maovu wala tusiwaonee aibu, tunatakiwa kuwakemea ndani ya kanisa wale unaowajua wanafanya maovu ila kama watenda maovu wako nje ya kanisani tunatakiwa kuwafundisha na kuwaleta kwa Yesu.

Watu wanaoiba maofisini, wanashindwa kulipa madeni na kuhama mitaa kutokana na madeni, hao tunapaswa kuwakemea kama watu tuliokoka na tunayetamani kwenda mbinguni. Mungu anasema hao walioko ndani (waliokoka na wanamjua Mungu) ya kanisa usile nao wala kukaa nao kama wanatenda maovu.

Mungu anasema, enyi wasinzi, acha usinzi, waimbaji acheni uzinzi-mnaweza mkawa mnaimba vizuri kutuburudisha lakini mkakosa mbingu. Kumbukeni huo mwili ni hekalu la Roho Mtakatifu. Biblia inasema, hata kula tusile nao, watu wa Mungu acheni dhambi!!! Wale ambao hawamjui Mungu na wanatenda dhambi Mungu anasema atashughulika nao, lakini wanaomjua na wanatenda dhambi Mungu anasema, tusichangamane nao.

Maisha ya hapa duniani, ni maisha ya upepo, yataisha, sio mahali pa kuishi milele, tutanyauka. Maisha ya hapa dunia ni maisha Fulani ya majuto na mateso. Ukitembea katika njia ya Bwana, vitu unavyotaka utapata. Nabii Josephate Mwingira hapo zamani alikuwa choka mbaya mpaka watu wakawa wanamwita Pepsi kutokana na kuvaa nguo zake zilezile, lakini sasa hivi anachagua ni suti gani ya kuvaa, nah ii ni matokeo ya kumtumikia Mungu kwa uamnifu. Havianzi vitu bali Roho Mtakatifu kwanza na vingine baadae

Bingo yako huanza hapahapa duniani kabla ya kufa. Ukishakufa kinachofuata ni kuchagua njia ipi ya kwenda, kulia au kushoto na ni hukumu.

Mimi huwa nashangazwa sana naposikia watu wanasema “Mungu mlaze mwili wa marehemu mahali pema peponi” kama marehemu hakutengeneza maisha yake hapa dunia, maombi hayo ni kazi bure kwa Mungu.

Yesu yuko malangoni, anakuja, anakutamani, anataka kukupumzisha mzigi ulionao, ili upumzike. Mzigo unaweza kuwa wa uasherati, uzinzi, uongo, wizi n.k. Toa mizigo yakoinayokuelemea. Tunachukia sana uasherati kwani ni mbaya sana na unahusisha mwili wako moja kwa moja, dhambi zote ni sawa na ni mbaya, lakini ya uzinzi ni mbaya zaidi, inaharibu hekalu la Mungu.

wewe ni wa thamani sana na Mungu anakutamani lakini wewe unatenda dhambi na kuona tamu, Acha tama kwani ni mbaya inaweza kukusababishia kutamani kitu na ukitatumia njia zisizo halali na ukashitukia unatenda dhambi.

Mafanikio au utajiri ni mzuri sana lakini pia katika njiaza kumpendeza Mungu kuupata huo utajiri au mafanikio. Utajiri utakusaidia nini kwa kuua ndugu zako ili uwe tajiri, acha tama ndugu yangu!!

Tunasafiri sisi hakuna mji wa kudumu hapa duniani, Magari, majumba ya kifajhari ni ya hapa hapa duniani. Tutafute Mungu na kukaa na Yesu vizuri. Tusome mathayo 3:12, moyo wako uwe tayari kupokea na kusikia masomo ya maarifa. Soma Mathayo 23;17-18, moyo wako usitamani wenye dhambi, bali kumcha Bwana mchana kutwa, bila shaka kuna dhawabu. Soma Isaya 35:8-9, iko nia kuu kwa hao wasifio, njia ya watakatifu, wasio safi hawatapita njia hiyo kwani njia ya kwenda kwa Baba. Acha yale yanayomkosea Mungu.

Mungu awabariki.

Comments

hope said…
do aisee hakuna kitu nacho mshukuru mungu kama kunipa baba wa kiroho ambaye anapo fundisha neno lake namuwelewa na kumpenda zaidi mungu kwa kweli mimi nampenda sana mungu kwa kunipa mtume na nabii anaye niwezesha kuelewa neno katika biblia linasema nini

asante yesu kwa kunichagua

haleluya!!