RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

RUMA AFRICA INAKUPONGEZA MWANAFUNZI WA CHEMSHA BONGO NA BIBLE KWA KUFANYA MTIHANI WA MWISHO WA MWEZI

Mwandishi: Rulea Sanga.

RUMA AFRICA inakushukuru sana wewe ambaye umefanya mtihani ambao tunaamini ulikuwa mrahishi sana kwako kutoka na juhudi ulizonazo katika kusoma Neno la Mungu.

Ni imani yangu kuwa wewe uliyefanya huo mtihani, Mungu ataenda kufanya jambo fulani katika maisha yako. Huwezi kupoteza muda wako na kuumiza kichwa chako kwa kazi ya Mungu na YEYE akakuacha jinsi ulivyo. Mungu wetu ni Mungu wa huruma sana, na ni MUNGU ambaye hapendi kuona kijana wake anayefanya kazi yake kwa kujituma akaabishwa.

Ruma Africa inakupongeza sana mdau wa blogu hii kwa kufanya mtihani huu. Ipo siku utakuja kunitumia ujumbe baada ya kuona mafanikio kutoka na nguvu zako ulizowekeza katika kazi ya Mungu. Mungu atakulipa hapahapa duniani kabla ya kuonana naye huko mbinguni.

Tunakuomba uzidi kufanya kazi ya Mungu, na kuwa mshabiki sana katika mambo ya Mungu. Hebu fikiri mtu akiwa mshabiki wa kazi yako unajisiaje? Nadhani utajisikia vizuri sana na kuona unapendwa, Mungu naye ndivyo anavyojisikia.

Mimi nakupenda sana hata kama hunijui ila Mungu anakujua vyema. Sihitaji kukujua sana ila nahitaji kuona Mungu wangu anakujua sana.

Kwa wewe uliyefanya mtihani unaweza kuangalia majibu ya mtihani kwa kubofya hapa: http://rumaafrica.blogspot.com/p/chemsha-bongo-na-bible.html

ASANTE SANA

Comments